This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Thursday, May 2, 2013

HOTUBA YA MHESHIMWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE KILELE CHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI, MEI MOSI 2013, MBEYA

RAIS JAKAYA KIKWETE

Ndugu Nortiburga Maskini, Kaimu Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania;
Mheshimiwa Gaudensia  Kabaka (Mb),Waziri wa Kazi na Ajira;
Mheshimiwa Celina Kombani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi,
Mheshimiwa Hawa Ghasia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI;
Mheshimiwa Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya;
Ndugu Alexio Musindo, Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki;
Ndugu Nicholaus Mgaya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi;
Dkt. Aggrey Mlimuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE);
Waheshimiwa Mabalozi;
Mheshimiwa Jaji Regina Rweyemamu, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi;
Wenyeviti na Makatibu wa Vyama vya Wafanyakazi;
Viongozi na Watendaji Wakuu wa Serikali;
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya;
Wawakilishi wa Vyama vya Siasa;
Waheshimiwa Wabunge;
Ndugu Wafanyakazi na Wananchi;
Mabibi na Mabwana:


Shukrani
Niruhusuni nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutuwezesha kukutana hapa mjini Mbeya kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi kwa mwaka 2013.    Nakushukuru sana Ndugu Nortiburga Maskini, Kaimu Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) na viongozi wenzako kwa kunialika nije kuungana na wafanyakazi wenzangu kuadhimisha siku hii adhimu na ya kihistoria duniani.   Shukrani nyingi nazitoa kwa Mheshimiwa Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na wananchi wa Mbeya kwa kutupokea vizuri tangu tulipowasili.  Asanteni sana kwa ukarimu wenu.
Vile vile nawapongeza viongozi wa Mkoa huu na wa Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA) kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizi.  Kazi ya kuandaa sherehe kubwa kama hii sio ndogo.  Wenzetu hawa wameifanya kwa mafanikio makubwa kama sote tuliopo hapa tunavyoshuhudia.  Kwa niaba ya wafanyakazi wote nchini naomba mpokee shukrani zetu nyingi kwa kazi nzuri mliyofanya.
Umuhimu wa Siku ya Wafanyakazi Duniani
Kwa namna ya pekee nawapongeza sana wafanyakazi kote nchini kwa kuadhimisha siku hii.  Ni siku ambayo wafanyakazi duniani kote wanakumbushana umuhimu wa mshikamano na umoja katika kudai na kutetea maslahi na maendeleo yao.  Kwa ujumla ni siku ambayo wafanyakazi wanaungana pamoja kutafakari mustakabali wao.  Wafanyakazi wa Tanzania wanayo kila sababu ya kuisherehekea na kuienzi siku hii adhimu.  Ni siku yao ya kufanya tathmini ya jinsi wanavyotimiza wajibu wao wa kutoa huduma na kuzalisha mali pamoja na kutambua changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya kuzikabili.
Pongezi kwa Wafanyakazi Bora
Ndugu Kaimu wa Rais wa TUCTA;
Ndugu Wafanyakazi;
Nawapongeza wafanyakazi wote waliopewa tuzo ya kuwa wafanyakazi bora katika sehemu zao za kazi. Hongereni sana kwa mafanikio haya. Nina uhakika kwamba wapo wafanyakazi wengine wengi ambao wanafanya kazi kwa bidii katika maeneo yao ya kazi lakini hawakubahatika kupata tuzo. Naomba wasikate tamaa, waendelee kuchapa kazi.  Huenda na wao watabahatika Mei Mosi ijayo.  Napenda kutumia nafasi hii kuwakumbusha wafanyakazi wote kufanya kazi kwa bidii, umahiri na weledi ili kuongeza tija kwenye maeneo yao.  Mnayo nafasi kubwa ya kuchangia maendeleo ya nchi yetu na watu wake.  Nawaomba muitumie vizuri nafasi hiyo.
Kauli Mbiu ya Mwaka Huu
Ndugu Wafanyakazi;
Nawapongeza sana kwa Kauli Mbiu ya sherehe za mwaka huu isemayo “Katiba Mpya Izingatie Usawa na Haki kwa Tabaka la Wafanyakazi”.  Ni Kauli Mbiu yenye ujumbe maridhawa ambao umekuja wakati muafaka kabisa.  Nafurahi kwamba mmekumbuka jambo zito na lenye umuhimu wa aina yake kwa mustakabali wa wafanyakazi nchini.  Mimi na wenzangu wote Serikalini tunakubaliana na maudhui ya Kauli Mbiu hiyo. Katiba ya nchi ambayo haitajali haki za tabaka la wafanyakazi itakuwa na upungufu mkubwa sana.  Mimi binafsi naamini kwamba mambo muhimu ya wafanyakazi yatazingatiwa katika Katiba mpya.  Ni matumaini yangu kuwa wafanyakazi waliitumia vizuri fursa ya kutoa maoni katika hatua ya awali ya wananchi kutoa maoni yao na ile ya taasisi kutoa maoni yao.  Pia katika hatua za Mabaraza ya Katiba na Bunge Maalum, wafanyakazi watatoa maoni ya kuendeleza haki na maslahi yao ili yajumuishwe katika Katiba.
  Hata hivyo, ni vyema mkatambua kuwa Katiba haiwezi kubeba kila kitu kuhusu masuala ya wafanyakazi.  Baadhi ya masuala yanayohusu maslahi, usawa na haki za wafanyakazi yamefafanuliwa na yataendelea kufafanuliwa kwenye sheria husika kwa kuzingatia maazimio ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) na matakwa ya wafanyakazi na jamii.  Hakikisheni kuwa mnatoa mapendekezo yenu kuhusu sheria zilizopo ambazo zinahitaji kuboreshwa au mambo yanayohitaji kutungiwa sheria.  Nawahakikishia ushirikiano na msaada wangu na wa wenzangu Serikalini.
Risala ya Wafanyakazi
Ndugu Kaimu Rais wa TUCTA;
Ndugu Wafanyakazi;
Nimesikiliza kwa makini risala iliyowasilishwa kwa niaba yenu na Katibu Mkuu wa TUCTA, Ndugu Nicolas Mgaya. Ni risala ambayo imeandaliwa vizuri sana.  Imejitosheleza kwa hoja,  ina ushauri mzuri pamoja na mapendekezo ya kuboresha mishahara na maslahi ya wafanyakazi. Napenda kuwahakikishia kuwa tumepokea kwa mikono miwili ushauri na mapendekezo hayo.  Tutayafanyia kazi na tutapeana taarifa ya maendeleo yautekelezaje wake.
Nyongeza ya Mishahara
Ndugu Wafanyakazi;
Nawashukuru sana kwa kutambua juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali za kuboresha maslahi na mishahara ya wafanyakazi. Kazi hii tunaendelea nayo kila mwaka kulingana na ongezeko la tija katika uzalishaji na ukuaji wa uchumi. Kwa mfano, katika kipindi chetu cha uongozi, tumeongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma karibu kila mwaka.  Tulikuta kima cha chini kikiwa shilingi 65,000 tumekipandisha mpaka kufikia shilingi 170,000.  Katika mwaka ujao wa fedha (unaoanza Julai),  tunategemea kuongeza tena mshahara na kima cha chini cha mshahara wa wafanyakazi katika sekta ya umma.
Mambo hayo yanawezekana kutokana na mafanikio ambayo tumeendelea kuyapata katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali.  Tumefanikiwa kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kudhibiti ubadhilifu wa fedha za umma.  Kwa upande wa makusanyo ya kodi kwa mfano, mapato yameongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 541 kwa mwezi mwaka 2011/12 hadi kufikia shilingi bilioni 637 kwa mwezi mwaka 2012/13, ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.  Mapato yanapoimarika kama hivi, Serikali inakuwa na uwezo mkubwa wa kuwahudumia wananchi wake, kutekeleza miradi ya maendeleo  na wakati huo huo kuboresha zaidi maslahi ya wafanyakazi.
Pamoja na mafanikio hayo, lakini bado hatujafikia mahali ambapo tunaweza kuongeza mishahara kama vile ambavyo tungependa sote tupate.  Hata kwa kiwango cha sasa ambacho sote tunakubaliana hakitoshi bado mishahara inachukua sehemu kubwa ya mapato ya Serikali.  Kwa mfano, katika mwaka ujao wa fedha, Serikali inatarajia kutumia shilingi trilioni 4.76 kati ya shilingi trilioni 10.5 ya mapato ya ndani kwa ajili ya mishahara.  Kwa maana hiyo, katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha mishahara peke yake itachukua asilimia 44.9 ya mapato ya ndani. Lakini mishahara sio matumizi pekee ya fedha za Serikali.  Kuna majukumu mengine ya kuwahudumia wananchi na kutekeleza miradi ya maendeleo. Kwa sababu hiyo hatuwezi kutumia mapato yote ya Serikali au sehemu kubwa ya mapato hayo kwa mishahara peke yake.  Lazima pawe na uwiano mzuri kati ya matumizi ya mishahara na ya huduma muhimu ambazo Serikali inawajibika kutoa katika jamii.
Narudia kuyasema haya kuwahakikishia wafanyakazi kuwa Serikali kushindwa kuongeza mara moja mishahara kufikia viwango ambavyo sote tungependa iwe hakutokani na roho mbaya, dharau au kutokujali.  Bado uwezo hauruhusu kufanya hayo.  Inshalla muda si mrefu uwezo huo tutaufikia. Naamini hivyo kutokana na muelekeo wa ukuaji wa uchumi na hasa kama hakutatokea kutetereka kwa sababu yo yote ile.
Kuhusu kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi, Serikali imekamilisha utafiti kama ilivyoahidi.  Kinachosubiriwa ni bodi za kisekta za mishahara kujadili mapendekezo ya viwango vipya ili vianze kutumika mwaka ujao wa fedha.
Kima cha Chini cha Mshahara
Ndugu Wafanyakazi;
Katika risala yenu mmezungumzia suala la kupanga kima cha chini cha mshahara kitaifa.   Utaratibu huo tulikuwa tunautumia kabla ya kutungwa kwa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004 na Sheria ya Taasisi za Kazi Namba 7 ya mwaka 2004.  Utaratibu uliopo sasa wa kupanga kima cha chini cha mshahara kisekta una faida zake kwa wafanyakazi kwa sababu sekta zinatofautiana kwa uwezo.  Hivyo sekta zinatakiwa kulipa mishahara kwa mujibu wa uwezo wao wa kulipa.  Lakini, kama tunaona ipo haja ya kurejea utaratibu wa zamani wa kuwa na kima cha chini ya mshahara kitaifa, Serikali ipo tayari kujadiliana na wafanyakazi kuhusu jambo hili.  Nina uhakika muafaka juu ya suala hili utapatikana.
Punguzo la Kodi ya Mapato
Ndugu Wafanyakazi;
Kama mtakumbuka, suala la kupunguziwa kiwango cha kodi ya mapato inayotozwa kwa wafanyakazi nililizungumza mwaka jana, siku ya Mei Mosi mjini Tanga.  Nilisema kuwa mfumo huo wa kodi unazingatia kipato cha mfanyakazi ambapo kiwango cha kodi hupanda kadri kipato cha mfanyakazi kinavyopanda.  Vile vile, nilieleza kwamba mwaka 2007, Serikali iliamua kupunguza P.A.Y.E. (Pay As You Earn) kutoka asilimia 18.5 hadi asilimia 15 na mwaka 2010/11 ilipunguzwa tena na kufikia asilimia 14.  
Katika kikao chetu tulichokutana na viongozi wa TUCTA tarehe 27 Februari, 2013 tulijadili suala hili na kukubaliana kwamba Serikali iendelee kulichambua zaidi ili kutoa unafuu zaidi kwa wafanyakazi kila mwanya unapopatikana.  Nafurahi kuwaarifu kuwa kazi ya uchambuzi imekamilika na maombi yenu yamesikilizwa. Waziri wa Fedha atafafanua vizuri zaidi katika hotuba yake ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha wiki mbili zijazo.
Sekta ya Hifadhi ya Jamii
Ndugu Wafanyakazi;
Nawashukuru kwa pongezi zenu kuhusu maboresho ya sekta ya hifadhi ya jamii hapa nchini. Tumechukua hatua kama tulivyoahidi.  Katika kuboresha sekta hii,  Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imekamilisha tathmini ya afya ya kifedha ya mifuko yote.
Tathmini hiyo imeonesha kuwa mifuko yetu ya hifadhi ya jamii ipo kwenye hali nzuri kifedha na ni endelevu. Kwa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya malipo ya michango ya wanachama waliokuwepo kabla ya mwezi Julai 1999 mfuko ulipoanzishwa rasmi.  Kwa kuanzia, mwaka ujao wa fedha, Serikali italipa shilingi bilioni 50 ikiwa ni sehemu ya malipo hayo.  Napenda kuwatoa hofu wanachama wa Mfuko huo kuwa mafao yao yapo salama.  Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi.  Hakuna atakayestaaafu akakosa kulipwa mafao yake.
Vile vile Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kwa kushirikiana na Benki Kuu wameandaa na kutoa miongozo ya uwekezaji yenye lengo la kuiwezesha mifuko ya hifadhi ya jamii kufanya uwekezaji ulio salama na wenye tija unaomnufaisha mwanachama na taifa kwa ujumla. Tangu kuanza kutumika kwa miongozo hiyo Mei 2012, uwekezaji wa mifuko hiyo umeongezeka kutoka shilingi trilioni 3.38 mpaka shilingi trilioni 4.24. Pia mali za mifuko zimeongezeka kutoka shilingi trilioni 3.74 hadi kufikia shilingi trilioni 4.73.
Aidha, Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nazo zimefanyiwa marekebisho ambayo yanamwezesha mtu yeyote anayeingia kwenye ajira kwa mara ya kwanza kuchagua Mfuko wowote wa hifadhi anaoupenda na hivyo kuondoa ukiritimba uliokuwepo.  Natoa wito kwa waajiri kuheshimu uhuru huu wa mfanyakazi na kutomchagulia Mfuko wa kujiunga nao. Marekebisho hayo pia yameweka adhabu kali kwa Mfuko unaochelewesha kulipa mafao ya mwanachama.  Vile vile, napenda kuwafahamisha kwamba ile kero ya mwanachama kukosa au kupunjwa mafao yake kama amechangia mfuko zaidi ya mmoja imeondolewa.  Hivi sasa inawezekana mwanachama kuhamisha mafao yake kutoka mfuko mmoja kwenda mfuko mwingine.
Vyombo vya Mashauriano
Ndugu Wafanyakazi;
Kuhusu vyombo vya mashauriano vilivyopo kutatua madai ya wafanyakazi, ni vyema kutambua kuwa vimeundwa kisheria.  Na, utaratibu wa majadiliano uliopo baina ya Serikali na wafanyakazi upo kisheria. Pale unapokuwepo upande ambao haukuridhika na uamuzi ya vyombo hivyo, utaratibu unaruhusu kukata rufaa kwenye vyombo vya juu mpaka  Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Kazi.  Huu ndio utawala wa sheria ambao kila mwajiri, Serikali na vyama vya wafanyakazi vinao wajibu kuuzingatia. Pamoja na kusema hayo, tumepokea ushauri wenu wa kuitaka Serikali ichukue hatua kuimarisha zaidi utendaji na ufanisi wa vyombo vya mashauriano.  Tutafanya hivyo.
Vile vile tutaendeleza utaratibu wetu mzuri wa mashauriano tuliouanzisha yaani ule wa mimi kukutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kujadili kero za wafanyakazi.  Sote tunakubaliana kuwa utaratibu huu ni mzuri, hivyo tuwe tunakutana angalau mara tatu kwa mwaka. Tayari mwaka huu tumeshakutana mara mbili yaani tarehe 27 Februari, 2013 na jana tarehe 30 Aprili, 2013 tulikubaliana tutafute fursa mapema baada ya sherehe hizi tukutane.  Tutafanya hivyo.    
Madai Sugu ya Wafanyakazi
Ndugu Wafanyakazi;
Ninayo furaha kubwa kuwaeleza kuwa Serikali inaendelea kulipa madai ya muda mrefu ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa umma.  Hadi kufikia tarehe 30 Machi, 2013, watumishi 11,820 kati ya watumishi 52,039 wamelipwa malimbikizo ya mshahara ya jumla ya shilingi bilioni 12.6. Watumishi 27,245 wenye malimbikizo ya jumla ya shilingi bilioni 16 watalipwa muda wowote kuanzia sasa.  Madai yao yameshahakikiwa.  Aidha, madai ya watumishi 12,974 yenye thamani ya shilingi bilioni 12.5 yapo kwenye hatua ya uhakiki baada ya hapo yataingizwa kwenye mfumo wa malipo.
Tunaendelea Kuimarisha Utendaji Serikalini
Ndugu Wafanyakazi;
Tunaendelea na mikakati ya kuimarisha utendaji kazi na uwajibikaji Serikalini ili wananchi wahudumiwe vizuri na kama inavyostahili.  Hivi karibuni tumeridhia kuanzishwa kwa mfumo mpya wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa maeneo ya kipaumbele ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.  Lengo letu ni kuboresha na kuharakisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.  Mfumo huo unatokana na mifano mizuri inayotumika katika nchi kadhaa duniani ambako umewaletea ufanisi mkubwa.  Kilicho chema huigwa.    
Kwa hapa nchini, tutaunda chombo maalum kitachokuwa chini ya Ofisi ya Rais kuratibu mfumo huu mpya wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.  Tumeamua kuanza na maeneo sita ambayo ni utafutaji wa mapato, kilimo, maji, elimu, nishati na uchukuzi.  Ni matumaini yetu kuwa mfumo huu utakapoanza kutumika, utendaji  kazi na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali  utaimarika sana katika maeneo hayo.
Vile vile tunaendelea kuimarisha taasisi zetu zenye majukumu ya kusimamia nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma ili ziweze kutekeleza vizuri kazi zao na kwa ufanisi zaidi. Taasisi hizo ni pamoja na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, TAKUKURU, Tume ya Maadili ya Viongozi na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA).    
Ukuzaji wa Ajira Nchini
Ndugu Wafanyakazi;
Kama ilivyo kwa nchi nyingi duniani, nchi yetu inaendelea kukabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira ambapo waathirika wakubwa ni vijana na wanawake. Ukosefu wa ajira hapa nchini umefikia asilimia 12.    Kwa kutambua ukubwa wa tatizo, Serikali imekuwa inachukua hatua mbalimbali kuongeza fursa za ajira nchini.    Hatua hizo ni pamoja na kuboresha mazingira ya uwekezaji ili vitega uchumi viongezeke ili ajira zongezeke.  Pia tunapanua fursa za elimu katika ngazi zote na kuhimiza mafunzo ya ujasiriamali na ufundi.  Aidha, Serikali inaendelea kukuza na kuimarisha programu za kuwawezesha vijana kujiajiri wenyewe.
  Inatia moyo kuona kuwa juhudi hizo zinaanza kuzaa matunda.    Kwa mfano, kati ya Julai 2012 hadi Machi, 2013 jumla ya fursa za ajira 199,578 zimepatikana.  Nafasi 142,832 zilitokana na miradi ya maendeleo na nafasi 56,746 ni katika fani mbalimbali kwenye utumishi wa umma.   Aidha, kati ya Januari na Machi 2013, jumla ya nafasi za kazi 2,562 zimetangazwa na sekta binafsi iliyo rasmi kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Katika mwaka wa fedha 2013/14 Serikali itaendelea kuongeza fursa za ajira katika sekta mbalimbali hususan kwenye elimu, afya na miradi ya maendeleo itakayotekelezwa. Kati ya mwaka 2013/14 – 2015/16, Serikali imeandaa programu ya kukuza ajira kwa vijana itakayowezesha kupatikana kwa fursa za ajira 600,000.
Ndugu Wafanyakazi;
Kuhusu kuwezesha vijana kujiajiri, Serikali inaendelea kuchangia mifuko maalum ya mikopo na misaada kwa vijana na wanawake kupitia bajeti ya Serikali.  Tumeamua kuelekeza nguvu kwa vikundi vya vijana na wanawake waliojiunga pamoja kwa lengo la kufanya shughuli za uzalishaji mali na huduma.  Kuanzia Januari hadi Machi 2013, Serikali imetambua vikundi vya vijana wajasiriamali 502 kutoka mikoa 17 ya Tanzania bara vinavyohitaji mitaji. Vikundi hivyo vina jumla ya wanachama 5,385 (Wanawake 2,519 na wanaume 2,866). Kazi hii inaendelea katika mikoa mingine iliyosalia. Hatua itakayofuata itakuwa kuwawezesha kwa mitaji na mafunzo ili waweze kujiajiri katika shughuli mbalimbali za biashara na uzalishaji mali.  Napenda kutumia fursa hii kuwataka vijana ambao hawajaajiriwa kujiunga katika vikundi vya ushirika ili iwe rahisi kuwajengea uwezo wao wa kufanya shughuli za uzalishaji.
Naomba uongozi wa mikoa na wilaya nchini utenge maeneo maalumu yatakayowezesha vijana kufanya shughuli za uzalishaji na biashara. Hii ni pamoja na kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji ili vijana walio tayari kujiajiri katika shughuli hizo wapewe.  
Pia natoa wito kwa makandarasi na taasisi za umma na binafsi kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutoa fursa kwa vikundi vya vijana.  Nawapongeza sana Shirika la Nyumba la Taifa na VETA kwa kubuni mpango ambao utawasaidia vijana 5,000 kutengeneza na kuuza matofali kwenye miradi ya ujenzi wa nyumba za NHC.  Shirika la Nyumba la Taifa limeonesha njia, wengine nao wajitokeze kuwasaidia vijana wanaotaka kujiajiri.
Mabilioni ya JK
Ndugu Wananchi;
Tunakamilisha  taratibu za kuwekeza fedha zaidi katika Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi (Maarufu kwa mabilioni ya Bwana Fulani).  Tutaweka utaratibu mzuri zaidi utakaofanya mfuko kuwa endelevu na kunufaisha zaidi walengwa.  Katika miaka mitano ya uhai wa Mfuko huu tumejifunza kasoro mbili ambazo zitarekebishwa katika utaratibu mpya.  Kwanza kwamba waliofaidika na mpango huo hawakuandaliwa ipasavyo.  Na, pili, hapakuwepo na utaratibu mzuri wa kufuatilia na kupima matokeo yake.   Kasoro hizo zitaepukwa safari hii.
Bahati nzuri programu inayotekelezwa na Wizara ya Kazi na Ajira kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) na Benki ya CRDB kwa vijana waliohitimu vyuo vya elimu ya juu nchini ili waweze kujiajiri katika sekta ya kilimo na ufugaji inatoa mwongozo mzuri wa namna bora ya kuboresha Mfuko huo.  Katika programu hii, vijana wanaopewa mikopo, kwanza hupatiwa mafunzo ya ujasiriamali kisha ndipo hupatiwa mikopo.  Utaratibu huo umeonyesha mafanikio makubwa.  Vijana hao wameweza kujiajiri katika shughuli za kilimo, ufugaji na usindikaji wa chakula na mafuta.   Aidha, kutokana na shughuli zao hizo wameweza kutengeneza fursa nyingi za ajira kwa watu wengine.
Ndugu Wananchi;
Kufuatia mafanikio hayo, nimeyakubali maombi kwa Serikali kuidhamini programu hii.  Nimeitaka Wizara ilete Serikalini mapendekezo hayo tuidhinishe rasmi.  Kufuatia mafanikio hayo nimeelekeza utaratibu wa program hii utumike kwa Mifuko ya Vijana, Wanawake na ule wa Uwezeshaji wa Wananchi.
Mikopo ya Nyumba kwa Wafanyakazi
Ndugu Wafanyakazi;
Mwaka wa jana niliunda Kamati Maalum au kwa lugha maarufu Kikundi Kazi kikiongozwa na Gavana wa Benki Kuu na kushirikisha Mifuko ya Pensheni na Shirika la Nyumba la Taifa kutoa mapendekezo juu ya namna ya kuanzisha mpango wa mikopo ya nyumba kwa wafanyakazi.  Lengo langu ni kutaka tutengeneze mfumo wa kuwawezesha wafanyakazi kupata mikopo yenye masharti nafuu ili waweze kununua au kujenga nyumba.
Nimearifiwa kuwa Kikundi Kazi kimekamilisha kazi hiyo na wako tayari kunikabidhi mapendekezo yao.  Tutayafanyia kazi kwa wakati muafaka na tutaarifiana mpango utakuwaje.  Naamini mpango huu ukifanikiwa utakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wafanyakazi na utaongeza ari ya kujituma.
Maendeleo ya Mkoa wa Mbeya
Ndugu Wafanyakazi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu nina mambo mawili ya kuzungumzia.  Jambo la kwanza,  ninalopenda kulizungumzia ni masuala ya maendeleo ya Mkoa.  Nafurahi kwamba ndoto ya Kiwanja cha Ndege cha Songwe imetimia.  Bado kazi chache ambazo tutazikamilisha miezi michache ijayo.  Kinachofuata sasa ni matumizi ya kiwanja hicho.  Tumejenga kiwanja hicho ili kisaidie kuchochea ukuaji wa uchumi hasa kilimo cha maua, matunda na mboga kwa ajili ya kuuza nchi za nje.  Nimeshatoa maelekezo kwa viongozi wenu, kilichobakia ni ninyi kujipanga na kutumia fursa hii.  Suala la maji kwa jiji la Mbeya limekamilika, tumekata mzizi wa fitina.  Nimewaomba mhakikishe usalama wa mradi huo na mtafute vyanzo vingine vya maji siku za usoni.  Ujenzi wa barabara ya Mbeya – Lwanjiro – Chunya – Makongorosi unaendelea na tutahakikisha hausimami.  Tunajiandaa kutekeleza ahadi za barabara ya Kikusya – Itinda - Matema Beach, Itumba – Mbambo – Tukuyu; Mpemba – Isiongole - Ileje na Mbalizi – Mkwajuni - Chunya. Soko la Mwanjelwa linalojengwa baada ya lile la awali kuungua limekaribia kukiamilika.  Na, soko la Uhindini litajengwa kama la Mwanjelwa na kwa udhamini wa Serikali Kuu.   Nimepokea kilio chenu kuhusu ukubwa wa Mkoa, tutalifanyia kazi.
Amani na Usalama wa Nchi
Ndugu Wafanyakazi;
Pili, ni suala la upendo, amani na mshikamano miongoni mwetu.  Hili ni suala ambalo nimekuwa nikilizungumzia mara kwa mara. Napenda kuchukua nafasi hii tena kusisitiza kwamba sisi wote tunao wajibu wa kudumisha tunu hizi tulizorithi kutoka kwa waasisi wa taifa letu.  Tusikubali kuichezea wala kuipoteza amani tuliyonayo.  Ikipotea ni vigumu kuirudisha na inaweza isirudi na Tanzania haitakuwa tena kisiwa cha amani.  Wanasiasa, viongozi wa dini, wafanyakazi, wakulima na wananchi kwa ujumla wanao wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa nchi yetu inabaki kuwa nchi ya amani na utulivu. Tuwe wepesi kuyatambua na kuyaeupuka mambo yatakayosababisha uvunjifu wa amani, upendo na mshikamano miongoni mwa wananchi wa nchi hii.
Kwa upande wetu, mimi na wenzangu Serikalini tumeanza mazungumzo na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali kujadili namna ya kumaliza tofauti zilizoanza kujitokeza siku za hivi karibuni.  Tumepiga hatua ya kutia moyo na bado tunaendelea mbele.  Jambo linaloleta faraja ni kwamba wote wameona tulikokuwa tunaelekea siyo kuzuri na kwamba tufanye kila tuwezalo tuepukane nako.
Sisi Serikalini tutaendelea kuzungumza na viongozi wa dini wa pande zote na kuwaunganisha ili kuona maelewano yanarejea kama ilivyokuwa zamani.  Watanzania tuendelee kuishi bila kubaguana au kuchukiana kwa dini zetu.  Tutaendelea kuwa macho na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kuchochea vitendo vya uvunjifu wa amani bila kujali nafasi walionazo kwenye jamii, itikadi ya sisasa na dini waliyonayo.
Hitimisho
Ndugu Wafanyakazi;
Mwisho, napenda kurudia tena kuwahakikishia kuwa kila jambo mlilolitaja kwenye risala yenu tutalifanyia kazi. Ni wajibu wetu kuwasikiliza, ni wajibu wetu kushughulikia masuala yenu, na ni wajibu wetu kushirikiana nanyi ipasavyo.  Tunatambua umuhimu wa wafanyakazi kwa maendeleo ya taifa letu.  Mimi nawaahidi ushirikiano wangu binafsi na ule wa wenzangu wote serikalini wakati wote.  Tujenge nchi yetu kwa pamoja.
Nawashukuru tena Viongozi wa TUCTA kwa kunialika kwenye sherehe hizi muhimu.  Nawashukuru wafanyakazi pamoja na wananchi kwa kujitoleza kwa wingi.   Hongereni kwa sherehe zilizofana sana.  Sasa twendeni tukafanye kazi.
                          Asanteni kwa Kunisikiliza

Sunday, April 21, 2013

KINANA AISHUKIA CHADEMA LEO MJINI MOROGORO

*Asema viongozi wake wamekubuhu wa ubinafsi
*Wanajali maslahi binafsi ya Chama chao badala ya Watanzania
*Awatakja Watanzania kuwapuuza
Kinana akihutubia mjini Morogoro leo.Picha: Bashir Nkoromo
NA BASHIR NKOROMO, MOROGORO
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameisasambua Chadema na kusema ni chama ambacho daima kimekuwa kikiweka mbele maslahi yake binafsi kuliko ya Watanzania.

Amesema viongozi wa chama hicho wamekubuhu kwa udikteta kiasi cha kujiona wao ndio wanajua kila jambo kuliko watu wengine hata mwenzao wa chama cha upinzani ikitokea ana mawazo  au msimamo wasioutaka au ameipongeza serikali kwao huonekana ni msaliti na kibaraka wa CCM.

Akihutubia leo mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika jana mjini hapa,Kinana, alisema kuwa Chadema ni balaa kwa nchi naa watu kwani viongozi wake wamekuwa ni watu wa kuhubiri machafuko badala ya mshikamano uliozoeleka Tanzania.

Alisema kutokana na umangimeza wao sasa Chadema kimeanza kuigawa nchi kwa kutumia sera ya ukanda licha ya kwamba sera hiyoi ni kinyume cha katiba ya nchi na watu wake.

"Ninapenda leo niwaelezeni ndugu Watanzania Chadema ilivyojawa na ubinafsi, wamekuwa wakiwakukusanya Watanzania na kuwagawa kwa sera yao ya majimbo. hili si mara ya kwanza maana katika kipindi cha siku za hivi karubuni walitangaza wazi kuigawa nchi kwa kutaka
kujitenga kanda ya Kaskazini eti ili iwe chini ya utawala wao", alisema Kinana.

Kinana alisema CCM kama chama kilichoingia mkataba na Watanzania haiwezi katu kukaa kimya na kuona hali hii ikitokea, kila mara tumekuwa tukihubiri amani na mshakamano lakini Chadema hili limewashinda jambo ambalo alisema ni dalili kwamba viongozi wa Chadema wameingia katika siasa kwa malengo yao binafsi.

"CCM itaendelea kusema ukweli kwa kila jambo na wala haitaficha hata likiwa siyo la kufurahisha wanachama wake ili mradi ni la kweli, tofauti na  hawa Chadema, lazima Watanzania muwe makini nao kutokana na aina ya siasa na matendo yao wanayojinasibvu nayo" alisema Kinana.

Vurugu za Chadema
Kinana alisema kuwa Chadema wamekuwa ni watu wa maajabu na vurugu kubwa nchini, na katika hilo alitoa mfano ya mambo ambayo wanayafanya bungeni.

"Chadema kazi yao ni vurugu tu, utadhani wao ndio wamekuwa kambi ya upinzani wa kwanza bungeni katika nchi  hii. Walikuwepo wapinzani  kabla yao lakini kama CUF na Kina Mrema (Augustine Mrema) enzi za NCCR Mageuzi lakini hamkupara kushuhudia vituko kama

hawa Chadema ambao wanajiona wao ndio kila kitu. Wanatoa vitisho kila siku kwa Serikali hata kumtukana mkuu wa Nchi bila kujali kwamba ni kiongozi ambaye amefika pele kwa kuchaguliwa na idadi kubwa ya Watanzania", alisema.

"Wanabeza wapinzani wengine , wakiona mpinzani anapongeza kazi iliyofanywa na CCM wanaanza kumshambulia.Hakuna anayejua zadi ya Chadema .Wanamtukana Rais, wanaushambulia usalama wa Taifa, wanashambulia vyombo vya usalama,"alisema Kinana

"Hawa jamaa ni watu wa ajabu sana, kila kitu wanajua wao wengine hawajui.Wakigombana katika chama chao utasikia kuna mkono wa CCM. Sijui ni watu wa aina gani , wanafanya mambo ya ajabu sana kiasi cha kushangaza,"alisema.

Kinana alitoa ushauri kwa Chadema kuwa na uwezo wa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao kuliko kutumia muda wao mwingi kila jambo ambalo linakwenda kombo kunyoosha vidole kwa CCM.

"CCM tuna changamoto zetu nyingi, lakini tunatatua matatizo yetu wenyewe hatupotayari.Tuna makundi ndani ya chama lakini hayo ndio mambo ya siasa,"alisisitiza.

Mchakato wa Katiba mpya
Kinana alisema pamoja na kazi nzuri ambayo imefanywa katika mchakato wa Katiba mpya, kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ametoa hotuba yake ambayo inaonesha wazi hakuna ambacho kimefanyika katika mchakato huo.

Alisema kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe akiwa bunge ametumia muda wake mwingi kuzungumzia mchakato wa katiba mpya na kubwa katika hotuba yake kuwa haufai.

"Simsingizii kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni, ndani ya hotuba yake ameeleza wazi kuwa waliopewa dhamana ya kukusanya maoni ya Katiba mpya hawana ujuzi.Hii si kweli, waliopewa dhamana hiyo ni watu ambao wanaifanya kazi hiyo kwa uadilifu,"alisema.

Alisema Chadema ni watu binafsi ambao wao wametawaliwa na uroho mkubwa na wao kazi ni kuangalia maslahi zaidi na ni si maslahi ya nchi.

Ziara yake Morogoro
Kinana alisema kuwa ziara yake amejifunza mamb mengi lakini kubwa na msingi ambalo lipo kwa chama hicho kitahakikisha kinatafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi na hasa migogoro ya ardhi, mipaka na huduma za jamii ambazo nazo ni changamoto kubwa kwa maeneo mbalimbali.

"Ziara yangu na viongozi wengine wa chama chetu ambayo tuimefanya katika wilaya zote za Morogoro tumeona changamoto nyingi.Tumetafuta ufumbuzi wa matatizo lakini mengine yanapatiwa ufumbuzi baada ya kukaa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama na kisha kutoa maagizo kwa Serikali kutekeleza,"alisema.

Agizo kwa wabunge CCM
Katibu Mkuu huyo wa CCM, alitumia nafasi hiyo kwa kuwataka wabunge wa CCM kutembea kifua mbele kwani chama chao kinafanya kazi kubwa lakini aliwataka wawe makini na Chadema na kuwataka kutowasikiliza kwani sasa imetosha.

Alisema Chadema wamekuwa wakisikiliza muda mrefu ndani ya Bunge na kuna wakati wabunge wa CCM walichukia baada ya Rais Jakaya Kikwete kukubali kukutana nao kujadili mchakato wa Katiba Mpya.

Friday, March 8, 2013

UCHAGUZI WA KENYA: DONDOO ZA YANAYOJIRI


Shughuli ya kuhesabu kura za urais katika uchaguzi wa Kenya, inajikokota , huku ikizua hali ya taharuki katika nchi ambayo ingali na makovu ya ghasia za baada ya uchaguzi wake wa mwaka 2007.
Wagombea wakuu wa urais katika uchaguzi huo, Raila Odinga na Uhuru Kenyatta anayesubiri kesi yake katika mahakama ya kimataifa ya ICC, kufuatia tuhuma za kuhusika na ghasia za mwaka 2007.
Bwana Kenyatta yuko mbele kwa hesabu ya kura za urais dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga.
Upande wa Odinga unasema kwa hujuma imefanywa katika shughuli ya kuhesabu kura hizo katika ukumbi wa Bomas, viungani mwa Nairobi.
Uchaguzi ulifanywa chini ya katiba mpya iliyoundwa ili kuzuia kutokea tena kwa ghasia zizoshuhudiwa mwaka 2007, kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata...Hii imesemekana kuwa sababu moja ya wapiga kura kuchanganyikiwa

Kwa nini tume kachelewa kutangza matokeo?

Mfumo wa Elektroniki- uliotumiwa kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa Kenya. Mfumo huo uligoma siku ya Jumanne.
Hii haikumshangaza mwangalizi mkuu wa kikosi cha Jumuiya ya madola, Festus Mogae, rais wa zamani wa Botswana alisema kuwa, "bado hatujafikia kiwango cha nchi za Magharibi. ''

Shunguli ya kuhesabu kura ilikumbwa na changamoto kubwa kwani mitambo ya Tume ya uchaguzi iligoma
Hatujui kilichosababisha mitambo kugoma, lakini naibu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Lilian Mahirie alisema kuwa huenda mtambo ulivamiwa.
Na kwa sababu ya hilo, kura sasa zinahesabiwa kwa mikono moja baada ya nyingine.
Tume ya uchaguzi inatumai kuweza kumaliza shughuli hiyo na kutangaza matokeo rasmi Ijumaa, lakini kulingana na sheria ina hadi tarehe 11 kutangaza matokeo hayo.
Haya yote yanajiri wakati Kenya ikiwa inatumia mfumo mpya wa kuhesabu kura wa elektroniki ambao uligoma katika vituo vingi vya kupigia kura, na sasa wamelazimika kutumia sajili za wapiga kura.

Mzozo unatokana na nini?

Unatokana na kura ambazo zinasemekana kuharibika na hivyo haziwezi kuhesabiwa kama kura sahihi na ikiwa zinaweza kuhesabiwa sawa na kura zingine zisizo na makosa yoyote.
Muungano wa Bwana Odinga CORD unataka kura hizo kuhesabiwa lakini muungano wa Kenyatta JUBILEE umepinga hatua kama hiyo.
Mgombea mwenza wa Kenyatta, William Ruto ameteta akisema kuwa kupiga kura sahihi kunamaanisha kuweka kwenye kijisanduku kinachostahili, wakati, afisaa mkuu katika muungano wa Raila, Franklin Bett, amesema kuwa kura yoyote iliyowekwa katika sanduku la kura lazima iwe sehemu ya kura zote zilizopigwa.
Baadhi ya wagombea tayari wamejulishwa matokeo yao, hawa wakiwa magavana, maseneta na waakilishi wa wanawake
Wadadisi wanasema kuwa chini ya katiba mpya, kura sio lazima ziwe sahihi bora tu zimepigwa na kuingizwa ndani ya sanduku ya kura.
Wadadisi wanasema kuwa chini ya katiba mpya, kura sio lazima iwe sahihi ndio zihesabiwe, kura yoyote inaweza kuhesabiwa kinyume na mambo yalivyokuwa hapo nyuma.
Ikiwa pande hizo mbili zitakosa kusuluhisha mzozo huu basi huenda mmoja akalazimika kwenda katika mahakama kuu.
Swala hili ni muhimu kwa sababu katiba inasema kuwa ili kuzuia duru ya pili, mgombea lazima ashinde zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa katika duru ya kwanza na takriban asilimia 25 ya kura katika nusu ya kaunti zote.

Ni kura ngapi zilizoharibika zinazozozaniwa?

Hadi Jumanne , matokeo ya mwanzo yalionyesha kuwa idadi ya kura zilizoharibika ilikuwa asilimia sita, idadi ambayo ilikuwa nyingi kuliko kura alizopigiwa mgombea anayeshikilia nafasi ya tatu, Musailia Mudavadi.
Wadadisi wanasema kuwa kulikua na kura nyingi sana zilizoharibika kwa sababu wakenya walikuwa na mfumo mpya wa kupiga kura wakiwapigia kura wagombea sita na ndio maana wakachanganyikiwa sana.
Wapiga kura walimchagua rais, mbunge, mwakilishi wa wanawake, magavana, maseneta na mwakilishi wa kaunti
Ilipofika Alhamisi idadi ya kura zilizoharibika ilikuwa imeshuka pakubwa.

Mamilioni ya wakenya walijitokeza asubuhi na mapema kupiga kura
Haijulikani ni kwa nini.
Maafisa wa uchaguzi, sasa wanasema kuwa wamelegeza msimako kuhusu kura zilizoharibika, na sasa wanazijumlisha na kura sahihi hasa ikiwa iliwekwa kwenye sanduku isiyostahili mfano kura ya Gavana kuwekwa katika sanduku ya kura za rais.
Baadhi ya kura pia zilikataliwa kwa sababu alama aliyoweka mpiga kura kutoka nje kidogo ya boxi. Baadhi wanasema ikiwa nia ya mpiga kura inaweza kujulikana basi, kura hiyo inaweza kuhesabiwa.
Pia kumekuwa na mtafaruk kuhusu tofauti kati ya kura iliyokataliwa na kura sahihi.
Kulingana na sheria, kura inakataliwa ikiwa pamoja na mengine haina alama ya kuithibitisha kuwa kura sahihi.
Lakini kura iliyoharibika ni ile ambayo mpiga kura aliweka alama ambayo haistahili karibu na mgombea aliyetaka kumpigia kura. Kwa hili mpiga kura anaweza kuomba kura nyingine wakati ile ya kwanza aliyoiharibu ina kuwa kura inayokataliwa.

Je wakenya wamechukulia vipi kucheleweshwa kwa matokeo?

Wakati shughuli hii ikiendelea kucheleweshwa, ndio wakenya nao wanazidi kuwa na wasiwasi mkubwa, sababu ambayo inaweza kusababisha mgogoro mkubwa.
Siku ya Alhamisi mgombea mwenza wa Odinga, Kalonzo Musyoka, alisema kuwa kumetokea hujuma dhidi ya matokeo yao.
Milolongo mirefu ilishuhudiwa katika vituo vya kupigia kura
Awali,muungano wa Jubilee, ulituhumu Uingereza kwa kuingilia uchaguzi huo ili kumnyima ushindi, madai ambayo nchi hiyo imekanusha.
Kenyatta anakabiliwa na kesi ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya kimatifa ya uhalifu wa kivita, akihusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007 ambapo takriban watu zaidi ya 1,000 waliuawa na wengine laki sita kuachwa bila makao.
Kabla ya uchaguzi Muungano wa Ulaya ulisema utapunguza uhusiano na Kenya ikiwa itamchagua rais anayehusishwa na ICC, wakati naibu katibu wa Marekani kuhusu maswala ya Afrika, Johnnie Carson, alionya kuwa wakenya wajiandae kwa athari za kumchagua mtu fulani.

Nini umhumi wa Kenya Kimataifa?

Ina uchumi mkubwa wa Afrika Mashariki na hupokea msaada mkubwa kutoka nchi za Magharibi.
Shughuli ya kukusanya matokeo kura za urais imeanza upya zaidi ya masaa arobaini na nane baada ya wakenya kupiga kura
Pia ina jeshi lenye nguvu zaidi katika ukanda huo pamoja na kutuma maelfu ya wanajeshi nchini Somalia kupambana dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu.
Kwa hivyo, Ulaya na Marekani zinajipata katika hali ngumu kisiasa ikiwa Kenyatta anayekabiliwa na kesi ICC atachaguliwa kama rais mpya wa nchi.
Barani Afrika huenda kuchaguliwa kwake kusizue mtafaruku kwani muungano wa Afrika unaopinga mahakama ya ICC unamuunga mkono Rais Bashir wa Sudan ambaye anasakwa na mahakama hiyo.
Viongozi wa Afrika wameituhumu mahakama ya ICC, kwa kuwa na mapendeleo dhidi ya bara la Afrika na kupuuza makosa ya jinai yanayofanywa na viongozi wengine wa dunia.

Thursday, February 28, 2013

SADIFA AANZA ZIARA MKOA WA MOROGORO

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Hamis Sadifa
Vijana machacahari Mtela Mwampamba na Juliana Shonza walioihama Chadema hivi karibubi, wakiserebuka nje ya Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro, baada ya msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa,  Sadifa Hamis Juma kuwasili kwenye ofisi hiyo, Februari 28, 2013 kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo.
Sadifa akipatiwa burudani ya shairi na mmoja wa waghani maarufu wa mashairi mkoani Morogoro.Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda
Mwenyekiti wa UVCCM, Sadifa Hamis Juma akiwa na Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda wakati wa mkutano wa ndani kati ya Mwenyekiti huyo na wajumbe wa Baraza la Vijana mkoa wa Morogoro
Mkuu wa Utawala wa UVCCM Taifa, Abdallah Mpokwa akitoa utambulisho wa watu walioambatana na Sadifa kwenye msafara huo, katika ukumbi wa CCM mkoa wa Morogoro
Kada wa CCM aliyehamia kutoka Chadema hivi karibuni, Mtela Mwampamba akisalimia baada ya kutambulishwa ukumbini.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, Juma Borafya akisalimia baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho cha ndani. Wapili kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro mjini, Ali Issa, Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Taifa, Mfaume Kizigo na Sixtus Mapunda
VIVA VIJANA VIVAAAA!!!!!, Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Sixtus Mapunda akiongoza salaam maalum kwa Vijana wa UVCCM ukumbini. Pamoja naye kutoka kulia ni Katibu wa CCM Morogoro, Ali Issa na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Mfaume Kizigo. Walioketi kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Harrieth Sutta na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa.
VIVAAAA!!!, vijana wakiitikia salam ya Sixtus ukumbini, baadhi yao ni Shonza na Abubakar Assenga
VIVAAAA, VIVAAAA!!!!, Vijana wakiitikia  salam
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Morogoro Herieth Sutta akimkaribisha Sadifa kuzungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Sixtrus Mapunda
 NAFURAHI KUWA NA WEWE! Sadifa akimwambia Sixtus Mapunda kabla ya kuanza hotuba yake ya mkutano huo wa ndani uliofanyika Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro
Sadifa akizungumza kwenye mkutano huo wa ndani
Sadifa akisisitiza jambo
Na kusisitiza zaidi
Sadifa akizidi kusisitiza hotuba yake huku viongozi wakiwa makini kumzikiliza
ULIOCHAGULIWA MSIJIKWEZE, JISHUSHENI KWA WANACHAMA", Anasema Sadifa
 "Wapendeni waliowapinga wakati wa uchaguzi" msiwanunie, kama mtu hakukuunga mkono leo kwa hili ipo siku atakuunga kwa jengine", akasema
Sadifa akitoka na wenyeji wake ukumbini

Tuesday, January 1, 2013

MGEJA: MBOWE AMEVUNJA DEMOKRASIA


SHINYANGA, Tanzania 
   KAULI iliyotolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe  kwamba Dkt. Wilbroad Slaa ndiye atakayekuwa mgombea urais mwaka 2015 imetafsriwa kuwa ni uvunjaji wa demokrasia ndani ya chama hicho .

  Kauli hiyo imeelezwa kuwa inapingana na dhana nzima ya demokrasia nchini na kwamba Mbowe ameonesha wazi kwamba CHADEMA si chama cha kidemokrasia kama kinavyojieleza na kujinadi kila siku mbele ya watanzania na badala yake kinaendeshwa kifamilia.

  Akizungumza na viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini na wazee wa mjini Kahama juzi katika hafla fupi ya kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 katika ukumbi wa Kahama Hotel mjini hapa,. mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja alisema taasisi yake imeshitushwa na kauli hiyo.

 Mgeja alisema haamini kwamba chama ambacho kinachohimiza kila siku suala la demokrasia nchini, mwenyekiti wake asimame hadharani na kumtangaza mwanachama fulani kwamba ndiye atakayekuwa mgombea wa nafasi ya urais badala ya maamuzi hayo kufanywa na vikao halali vya kikatiba. 

 Alisema Taasisi yake ambayo moja ya shughuli zake ni kuimarisha suala la demokrasia nchini na utawala bora imesikitishwa na kauli ya Mbowe na kwamba ameonesha jinsi gani chama chake kinavyokandamiza demokrasia ndani ya chama ambapo ameifafananisha kauli hiyo na kauli zinazotolewa na madikteta duniani.

  “Hii kauli ni katika jitihada za Mbowe kuikandamiza demokrasia ndani ya chama, ni wazi sasa CHADEMA kimepoteza mwelekeo, si muda muda mrefu kitasambaratika,”  

“Hizi ni njama za wazi za kutowapa nafasi wanachama wengine wasiweze kujitokeza kuomba na kugombea nafasi hiyo kupitia CHADEMA, sisi hatuamini kwamba Dkt. Slaa ndiye anayefaa peke yake, maana chama hicho kina watu wengi wanaoweza kujipima kuwania nafasi hiyo kama vile Zitto (Kabwe) na Shibuda (John),” alisema Mgeja.  

Mgeja ambaye pia  ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) na mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga alisema baada ya kauli hiyo sasa haitokuwa rahisi kwa wana CHADEMA wengine kama vile Zitto na Shibuda kuweza kuwania nafasi hiyo ambao tangu awali walitangaza nia ya kugombea. 

 “Kauli ya Mbowe sisi Tanzania Mzalendo Foundation tunaiita kuwa ni kauli ya kibabe na kidikteta na ambayo moja kwa moja inawapokonya haki yao ya kikatiba Zitto na Shibuda, hawatoweza tena kuitumia, maana tayari mwenyekiti wao Taifa ameishatoa msimamo wa chama,”

 “Nafikiri ni katika mbinu za kuwawekea vizingiti mapema, maana hata muasisi wa CHADEMA, Edwin Mtei amesikika akiunga mkono kauli ya Mbowe ambaye tunafahamu wazi kuwa huyo ni baba mkwe wake, na ni wazi kuwa msingi wa kauli hiyo ni kuwadhibiti Shibuda anayetokea kanda ya ziwa na Zitto anayetokea Kigoma,” alieleza Mgeja. 

 Hata hivyo Mgeja alimtaka Mbowe aelewe kuwa kauli yake hiyo mbali ya kuvunjavunja mfumo wa demokrasia nchini lakini pia inawanyima wanachama wengine wa CHADEMA haki yao ya kikatiba na kwamba kwa kufanya hivyo ameichezea katiba ya chama chake.

  Akizungumzia hali ya amani na utulivu uliopo hivi sasa nchini, Mgeja alisema ipo hatari ya hali hiyo kutoweka iwapo serikali haitochukua mapema hatua za kuwakemea wale wote ambao wameanza kueneza maneno ya uchochezi ambayo yanaweza kusababisha kutokea kuvunjika kwa utulivu uliopo.

  Alisema moja ya watu wanaoeneza maneno ya uchochezi ni viongozi wa CHADEMA ambao mara kwa mara katika mikutano yao wamekuwa wakitishia kuingia msituni pale watakapobaini matakwa yao yameshindwa na hawakuungwa mkono na watanzania. 

 Mgeja alisema kauli ya hivi karibuni ya viongozi wa CHADEMA kwamba mwaka 2013 Tanzania haitotawalika ni kauli hatarishi kwa amani na utulivu uliopo hapa nchini hivi sasa na kwamba inapaswa kukemewa vikali na kila mpenda amani. 

“Hizi kauli kwa kweli ni kauli hatari sana kwa mstakabali wa nchi yetu, haziendani na utamaduni wa watanzania, nchi yetu imezoea amani na utulivu na imekuwa na umoja wa kitaifa daima, na ni mfano wa kuigwa na mataifa mengine duniani,”

  “Ni vizuri zikakemewa na kila mtanzania, lakini hawa wenzetu pia wamekuwa na tabia ya kutoa kauli za zinazomdhihaki  Rais wa nchi aliyeko madarakani, ambaye alikula kiapo halali cha kuwatumikia watanzania wote bila ya ubaguzi wowote, huu ni utovu wa nidhamu, ni vizuri wakakemewa mapema,” alisema Mgeja. 

 Alisema inavyoelekea hivi sasa CHADEMA kimeanza kupoteza mwelekeo kiliokuwa nao na kinaelekea kuporomoka mporomoko mkubwa, na kwamba kinapoamua kuachana na demokrasia ndani ya chama kama lilivyo jina lake ni wazi wanachama watasambaratika haraka.  

“Ni wakati muafaka hivi sasa kwa watanzania kuchukua tahadhari kubwa na viongozi hawa wa CHADEMA, waache ile tabia ya kuwaunga mkono na kuingia mabarabarani kupinga mambo bila ya wao wenyewe (wananchi) kuchunguza sababu ya wao kuandamana, watajikuta  wakiwahangaikia watu wachache kwa maslahi yao binafsi,” alisema.

   Akizungumza katika hafla hiyo, Al Haji Alley Juma kwa niaba ya wazee wa mji wa Kahama alisema ni vizuri sasa Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa awe macho na kufuatilia kwa karibu kauli mbalimbali zinazotolewa na viongozi wa vyama vya siasa ambazo zinaweza kuchangia kuvunjika kwa haliya amani na utulivu.   uchochezi huku wakitoa maneno ya kumdhalilisha Rais, hawa wasiruhusiwe kuichezea amani tuliyonayo, wadhibitiwe mapema na ikibidi watajwe hadharani,” alisema mchungaji Mlekwa. 

Monday, December 31, 2012

HOTUBA YA RAIS KIKWETE KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA 2013

Utangulizi 
Ndugu zangu, Watanzania Wenzangu;
Ni furaha na faraja kubwa kuifikia siku hii adhimu ya kuuaga mwaka wa 2012 na kuukaribisha mwaka 2013. Ni jambo la bahati ambayo hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kuumaliza mwaka huu salama.  Wapo ndugu, jamaa na marafiki zetu wengi ambao wangependa kuiona siku hii lakini hawakujaaliwa. Wametangulia mbele ya haki.  Tuendelee kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape mapumziko mema.  Amin.   Nasi tumuombe Mola wetu atujaalie fanaka tele katika mwaka ujao.

Mapitio ya Mwaka 2012
Ndugu wananchi;
Mwaka tunaoumaliza leo ulikuwa wenye mambo mengi mazuri na mafanikio makubwa, lakini, pia, ulikuwa na changamoto zake. Baadhi zilikuwa ngumu na zipo zilizokuwa za kusikitisha na kuhuzunisha.
Ajali za barabarani na majini ziliendelea kupoteza maisha ya watu wengi na kusababisha majeraha na ulemavu kwa maelfu.  Ajali mbaya kuliko zote kutokea, mwaka huu, ilikuwa ile ya meli ya MV Skagit iliyotokea tarehe 18 Julai, 2012 ambapo watu 144 walipoteza maisha.  Ajali za barabarani zilizosababisha vifo nazo ziliongezeka kutoka 3,012 mwaka 2011 hadi kufikia 3,144 na kusababisha
vifo vya ndugu zetu 3,714.

Ndugu Wananchi;
  Kufuatia ajali ya MV Skagit ambayo ilitokea miezi 11 baada ya ile ya MV Spice Islander, Serikali zetu mbili zimekuwa zikishirikiana kwa karibu kuhusu masuala ya usafiri wa majini kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.  Kwa ajili hiyo SUMATRA na Zanzibar Maritime Authority zinafanya kazi kwa karibu zaidi na kanuni za usafirishaji wa abiria na mizigo na za usajili na ubora wa meli zimewianishwa.  Ni matumaini yetu kuwa hatua hizo zitasaidia kumaliza ajali zinazotokana na makosa ya wanadamu.

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa ajali za barabarani tuliendelea na tutaendelea kuwahimiza madereva kuheshimu Sheria za Usalama Barabarani, waepuke uzembe na hasa ulevi wakati wa kuendesha.  Tutaendelea kuwakumbusha wenye magari kuhakikisha kuwa uzima wa magari yao unakuwa wa kiwango cha juu.  Hali kadhalika, tumewataka Polisi waongeze ukali na kuwabana ipasavyo madereva na wamiliki wa magari ili watekeleze wajibu wao na wasipofanya hivyo wawajibishwe inavyostahili.

                                        Hali ya Usalama
Ndugu wananchi;
Tunaumaliza mwaka huu nchi yetu ikiwa shwari, salama na tulivu.  Tuombe Mungu hali hii iendelee mwaka 2013 na idumu milele.  Mipaka ya nchi yetu ipo salama na uhusiano na majirani na nchi zote duniani ni mzuri.  Tunaendelea kutafuta suluhu ya mgogoro wa mpaka kati ya nchi yetu na Malawi katika Ziwa Nyasa kwa njia ya mazungumzo. Suala hilo limewasilishwa kwa pamoja na Serikali zote mbili kwa Mheshimiwa Joaquim Chissano, Mwenyekiti wa Umoja wa Viongozi Wastaafu wa Afrika kwa ajili kuzisaidia nchi zetu kupata ufumbuzi.  Matumaini yetu ni kuwa viongozi hao watalishughulikia suala hili mapema iwezekanavyo.
Ushirikiano wa Kanda

Ndugu Wananchi;
Ushirikiano wetu wa kikanda katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) unaendelea vizuri.  Mwaka huu nchi yetu imepewa heshima kubwa ya kuwa Mwenyekiti wa Chombo cha SADC kinachoshughulikia masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama.
  Jukumu hilo ni zito na hasa katika kipindi hiki ambapo kuna changamoto za kisiasa na kiusalama katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Madagascar na Zimbabwe.  Nchi yetu inatarajiwa kuongoza juhudi za kupata ufumbuzi wa migogoro hiyo migumu.  Ndiyo maana tulifanya Mkutano  Maalum wa Wakuu wa Nchi za SADC hapa Dar es Salaam tarehe 7 na 8 Desemba, 2012.  Mwaka ujao, kwa kushirikiana na wenzetu, tutaendeleza juhudi zetu.  Ni matumaini yangu kuwa tukipata ushirikiano wa viongozi na wananchi wa nchi husika na jumuiya ya kimataifa tutapata ufumbuzi tunaotaka.

Ndugu Wananchi;     
Kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, tumeendelea kushuhudia Jumuiya hiyo na harakati za utangamano zikizidi kustawi.  Jengo la Makao Makuu ya Jumuiya limekamilika na kuzinduliwa rasmi tarehe 28 Novemba, 2012.  Siku hiyo hiyo kule Athi River, Kenya, barabara ya kutoka Arusha hadi Athi River ilizinduliwa.  Barabara hii ni moja ya miradi kadhaa inayotekelezwa kwa pamoja na nchi wanachama wa Jumuiya wa Afrika Mashariki.

Mchakato wa utangamano wa kiuchumi wa Afrika Mashariki unaendelea kwa kasi.  Tanzania ikiwa sehemu kamili ya mchakato huo, lazima tuhakikishe kuwa tunakwenda nao sambamba.  Tusikubali kuachwa nyuma wala kuwa chanzo cha kuuchelewesha mchakato huo bila ya sababu za msingi.  Utangamano una maslahi kwa nchi yetu na manufaa yake ni makubwa.  Kwa mfano, mauzo yetu katika soka la Afrika Mashariki yameongezeka sana kutoka dola za Kimarekani milioni 58.6 mwaka 2000 hadi kufikia dola za Kimarekani milioni 409 mwaka 2011.

 Jumuiya imekuwa kichocheo muhimu cha kukuza uzalishaji, ajira na uchumi hapa nchini.  Kwa ukubwa wa nchi yetu na rasilimali tulizonazo tuna matumaini makubwa ya kunufaika zaidi siku za usoni.  Naweza kuthubutu hata kusema kuwa Tanzania inaweza kunufaika zaidi kuliko nchi nyingine wanachama wa Jumuiya hiyo.  Kinachotakiwa ni sisi kujipanga vizuri kwa sera na mipango ili tuzitumie fursa tulizonazo kwa maslahi ya uchumi na maendeleo ya nchi yetu na watu wake. Tuache woga, tujiamini.

Matishio ya Usalama
Ndugu Wananchi;
Licha ya kumaliza mwaka nchi ikiwa shwari na yenye amani na utulivu, yalikuwepo matukio yaliyotishia usalama wetu.  Bahati mbaya na kwa masikitiko makubwa matukio hayo yalisababishwa na baadhi ya viongozi wa dini na siasa na wafuasi wao.  Kwa kweli kwa mara ya kwanza nchi yetu ilifikishwa kwenye hatari ya kutokea mgawanyiko mkubwa wa Watanzania au hata mapigano ya raia kwa misingi ya dini zao.  Bahati nzuri hilo halikutokea na Mungu aliepushe lisitokee kamwe.

Nimeshalisemea jambo hili siku za nyuma na napenda kurudia tena leo kuwasihi Watanzania wenzangu kupima athari za kauli zetu na matendo yetu kwa mustakabali wa jamii yetu, nchi yetu na watu wake.  Viongozi wa dini, waumini na viongozi wa siasa na wafuasi wao wanao wajibu maalum wa kuhakikisha kuwa Watanzania wanaendelea kuishi kwa upendo, amani na ushirikiano bila kujali tofauti ya dini zao, makabila yao, rangi zao au maeneo watokako.  Hiyo ndiyo sifa ya nchi yetu tunayoijua sote ambayo ni njema na watu wengi wanataka kuja kujifunza kwetu na wale wenye shida wanatamani wawe kama sisi.  Hii ni tunu muhimu ya taifa ambayo tusikubali kuipoteza kwa maslahi binafsi ya watu wachache.

Ndugu Wananchi;
Wakati wo wote, lazima tutambue umuhimu wa kuvumiliana na kuheshimiana kwa tofauti zetu za kidini, rangi, kabila, tutokako na ufuasi wa vyama vya siasa.   Lazima pia tuhakikishe kuwa tunaheshimu sheria na taratibu zinazotawala mikutano na maandamano.   Tukiyazingatia hayo nchi yetu itakuwa haina tishio lo lote kwa amani na usalama wake.  Yasipozingatiwa tunaiweka nchi yetu hatarini.  Sisi katika Serikali tutakuwa hatuna la kufanya bali kutimiza wajibu wetu wa kulinda usalama wa raia na nchi yetu.  Wahusika watachukuliwa hatua na vyombo vya usalama na kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi.  Tulifanya hivyo mwaka huu na hatutakuwa na ajizi kufanya hivyo siku yo yote kama hapana budi.

Uhalifu Unapungua
Ndugu Wananchi;
  Inatia moyo kuona kuwa mwaka huu makosa ya jinai yalipungua na kufikia 66,255 yakilinganishwa na makosa 69,678 ya mwaka jana au 94,390 ya mwaka juzi.  Hii inathibitisha kuimarika kwa kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Polisi wakishirikiana na wananchi na vyombo vingine vya usalama.  Pamoja na hayo lazima tuongeze juhudi za kupambana na uhalifu kwani bado matukio ni mengi mno na upungufu bado ni mdogo.  Tutaendeleza kazi tuifanyayo sasa ya kuliimarisha Jeshi la Polisi kwa rasilimali watu, zana na vitendea kazi husika.

Uhalifu wa Kimtandao
Ndugu Wananchi;
Tutaongeza nguvu katika kupambana na uhalifu unaoendeshwa na mitandao ya uhalifu ndani na nje ya nchi.  Mitandao hiyo hasa imekuwa inajihusisha na biashara ya kusafirisha wanadamu, biashara ya dawa za kulevya na biashara ya nyara za Serikali.

Mapambano dhidi ya uhalifu wa kimtandao yametuwezesha kukamata wahamiaji haramu 4,765 na tayari 1,611 wamerudishwa kwao.  Kwa upande wa dawa za kulevya watuhumiwa 6,929 walikamatwa mwaka huu ukilinganisha na 209 mwaka 2011. Kilo 55,285 za dawa za kulevya zilikamatwa mwaka huu ukilinganisha na kilo 17,752.4 mwaka jana.  Kwa upande wa nyara za Serikali, zilizokamatwa ni 1,416 na kati ya hizo 736 ni meno ya tembo.  Watuhumiwa 1,037 walikamatwa na kesi 746 zipo Mahakamani katika hatua mbalimbali.

Ndugu Wananchi;
Taarifa hizi zinathibitisha kuimarika kwa jitihada za kupambana na uhalifu wa kimtandao.  Tutaimarisha zaidi jitihada zetu mwaka 2013 ili tupate mafanikio zaidi.  Tutaviongezea uwezo wa rasilimali watu, zana, vifaa na fedha za uendeshaji vyombo vyetu vya usalama vinavyoongoza mapambano haya.

Tutaimarisha na kuendeleza ushirikiano baina ya nchi yetu na nchi jirani na nyinginezo duniani.  Hii itasaidia kutuongezea uwezo wa kupambana na mitandao ya uhalifu ndani ya nchi, kikanda na kimataifa.  Pia tutazipitia upya sheria za kupambana na makosa haya kwa nia ya kuziboresha.

Ndugu Wananchi;
Katika mwaka 2013, tutapanua na kuimarisha huduma ya matibabu kwa watu walioathirika na dawa za kulevya kote nchini.  Tutakamilisha ujenzi wa kituo cha Dodoma na kujenga kingine kipya Dar es Salaam.  Natoa wito kwa wale wote walioathirika au watu wenye watoto au rafiki au jamaa walioathirika waende hospitali kupatiwa matibabu kwani matibabu hayo ni bure.

Hali ya Uchumi
Ndugu wananchi;
Katika mwaka 2012, tunaoumaliza leo,  uchumi wa nchi yetu uliendelea kukua na kuimarika licha ya kuwepo kwa changamoto za upatikanaji wa umeme, kupanda kwa bei za mafuta na chakula duniani na uhaba wa mvua katika maeneo mengi nchini uliosababisha kupungua kwa uzalishaji na kupanda kwa bei za vyakula nchini.  Pia, licha ya kuendelea kwa msukosuko wa uchumi wa dunia na hasa katika Bara la Ulaya ambako ni soko kuu la bidhaa zetu na watalii.  Mategemeo yetu ni kuwa, mwaka huu, uchumi wetu utakua kwa asilimia 6.8 na  mwakani (2013) utakua kwa asilimia 7.0 ukilinganisha na asilimia 6.4 mwaka 2011.

Kwa jumla, ukilinganisha na makadirio ya IMF ya kiwango cha ukuaji wa uchumi wa dunia kuwa asilimia 3.3 mwaka huu, ni dhahiri kuwa uchumi wetu unakua kwa kasi nzuri na kuifanya Tanzania iendelee kuwa miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa.

Hali hii ya uchumi wetu ina maana kubwa mbili.  Kwanza, kwamba uchumi wetu umejenga uhimilivu dhidi ya misukosuko ya uchumi wa dunia.  Na pili, kwamba shughuli za uzalishaji na huduma zinazidi kukua na mauzo ya bidhaa ndani na nje ya nchi yameongezeka.  Kuongezeka kwa mauzo ya nje kumefanya akiba yetu ya fedha za kigeni kufikia dola za Marekani bilioni 3.9 mwezi Novemba, 2012 kiasi ambacho kinatuwezesha kuagiza bidhaa kutoka nje kwa miezi minne.

Ndugu Wananchi; 
Makusanyo ya mapato ya Serikali yatokanayo na kodi yalifikia shilingi bilioni 580.3 mwezi Oktoba, 2012 ikilinganishwa na shilingi bilioni 479.3 mwezi Oktoba 2011.  Matarajio yetu ni kufanya vizuri zaidi mwaka 2013 kwa mapato yatokanayo na kodi na yale yasiyotokana na kodi ambayo bado ni chini ya lengo.

Ndugu Wananchi;
Mfumuko wa bei kuwa juu ni changamoto ambayo tunaendelea kuikabili ili kuleta utulivu uliokamilifu kwa uchumi wetu na kuwapunguzia ukali wa maisha wananchi wa Tanzania.  Serikali imechukua hatua kadhaa kudhibiti hali hiyo na mafanikio ya kututia moyo yameanza kuonekana.  Kwa mfano, mfumuko wa bei umepungua kutoka asilimia 19.8 mwezi Desemba 2011 hadi asilimia 12.1 mwezi Novemba, 2012.  Kiwango hicho bado ni cha juu na hakikubaliki.  Tutaendelea kuchukua hatua zaidi ili tuweze kufikia lengo letu la mfumuko wa bei kuwa chini ya asilimia 10 ifikapo mwezi Juni, 2013.

Miongoni mwa mambo tuliyopanga kufanya ili kupunguza mfumuko wa bei ni kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme na kudhibiti mwenendo wa bei ya mafuta.  Kufanya hivyo kutasaidia kupunguza gharama za uzalishaji na uchukuzi wa bidhaa. Aidha, tutaendelea kutekeleza mipango na mikakati ya kukuza na kuboresha kilimo nchini kwa lengo la kujihakikishia usalama wa chakula, kukuza pato la taifa na kupunguza umaskini hasa miongoni mwa wakulima.

Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
Ndugu wananchi;
Mwaka huu tunaoumaliza leo ulikuwa na mafanikio ya kutia moyo kwa upande wa utekelezaji wa miradi ya kuendeleza miundombinu nchini.  Tumeshuhudia miradi ya barabara, madaraja, viwanja vya ndege, reli, bandari, umeme na maji ikikamilika, au kuanzwa au utekelezaji wake ukiwa unaendelea.  Hakika lengo la kuunganisha mikoa yote ya Tanzania Bara kwa barabara za lami siyo ndoto tena bali ni jambo la uhakika na litatimia muda si mrefu ujao.

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa reli, mwaka huu tumeendelea kukarabati reli ya kati na kurejesha usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na Kigoma.  Mwaka ujao (2013) tutaendeleza kazi ya ukarabati wa reli hiyo muhimu na kuzidi kuboresha huduma.  Tumekamilisha ujenzi wa viwanja vya ndege vya Mpanda na Songwe na tunaendelea kuboresha viwanja vya Tabora, Kigoma, Bukoba, Mafia, Mwanza na Zanzibar.  Tumeendelea kujenga na kupanua miundombinu ya maji nchini na kuboresha upatikanaji wa maji salama kwa Watanzania. Kwa mwaka huu usambazaji wa maji salama umefikia asilimia 87 kwa watu wa mijini na asilimia 61.5 vijijini.   Tutaendeleza kazi hiyo mwaka 2013.

Msongamano wa Magari Dar es Salaam
Ndugu Wananchi;
Katika Jiji la Dar es Salaam tumeendelea na tutaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kupunguza msongamano wa magari unaozidi kuongezeka.  Barabara mpya zimejengwa na zinaendelea kujengwa ndani na kuzunguka Jiji.  Barabara kadhaa zimepanuliwa na nyingine zitaendelea kupanuliwa.  Ujenzi wa miundombinu (barabara na vituo) ya mabasi yaendayo haraka umeanza.  Mwaka 2013 ujenzi wa barabara za juu ya nyingine katika makutano ya TAZARA utaanza na matayarisho ya kufanya hivyo kwa makutano ya Ubungo yatakamilishwa.
Tumetimiza ahadi yetu ya kutumia treni kusafirisha abiria katika jiji la Dar es Salaam.  Usafirishaji umeanza na unaendelea kati ya Stesheni na Ubungo na kutoka Stesheni ya TAZARA hadi Pugu – Mwakanga.  Mwaka ujao tutaendelea kuimarisha usafiri huo kwa kuongeza treni na idadi ya safari.  Tayari Mshauri Mwelekezi ameshateuliwa kufanya upembuzi yakinifu na kushauri kuhusu kupanua huduma hiyo mpaka ifike Tegeta, Bunju, Kimara, Luguruni, Kibaha, Mbagala-Rangi Tatu na Kongowe.  Ushauri huo pia utahusu kuwa na huduma bora ya usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam kwa maana ya aina ya njia, vichwa vya treni na mabehewa.  Tuliamua kuanza na reli na treni iliyopo, lakini nia yetu ni kufanya vile hasa inavyotakiwa iwe kwa usafiri wa treni mijini.
Umeme

Ndugu Wananchi;
Mwaka tunaoumaliza leo haukuwa rahisi kwa upande wa upatikanaji wa umeme.  Mabwawa ya kuzalisha umeme ya Kidatu, Kihansi, Mtera, Pangani na Nyumba ya Mungu yameendelea kutokuwa na maji ya kutosha kwa sababu ya uhaba wa mvua.  Hivyo basi taifa limelazimika kutegemea umeme wa kukodi unaozalishwa kwa kutumia mafuta.  Umeme huo umekuwa wa gharama kubwa na hivyo kuwa mzigo mkubwa kwa TANESCO na taifa. Serikali imeendelea kushirikiana na TANESCO na kuisaidia kubeba mzigo huo.  Tutaendelea kufanya hivyo mwaka ujao na mpaka tutakapofikia hatua ya kutokuwa na ulazima wa kutumia umeme wa kukodi.

Ndugu Wananchi;
Mtakumbuka kuwa tulipopata tatizo la ukame na upungufu wa umeme mwaka 2006/2007, Serikali yetu iliazimia kuongeza uzalishaji wa umeme kutokana na vyanzo vingine vikiwemo gesi asili, makaa ya mawe, upepo na jua.  Nafurahi kusema kuwa, tangu wakati ule Serikali imeiwezesha TANESCO kujenga vituo vitatu vinavyozalisha MW 245 kwa kutumia gesi.

  Hatukuweza kuongeza zaidi uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi kwa sababu ya kiasi cha gesi kinacholetwa Dar es Salaam kutoka Songo Songo kuwa kidogo.  Ndiyo maana tukaamua kujenga bomba jipya kubwa la kusafirisha gesi kutoka Songo Songo hadi Dar es Salaam.

Ndugu Wananchi; 
Kwa nia ya kutaka kuhakikisha kuwa kutakuwa na gesi ya kutosha kuzalisha umeme mwingi zaidi pale inapohitajika, ikaamuliwa bomba hilo liendelezwe mpaka visima vya gesi vya Mtwara.  Ujenzi wa bomba hilo umeanza mwezi Novemba, 2012 na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18.  Gesi itakayopatikana ina uwezo wa kuzalisha MW 3,000 za umeme.  Tayari mipango inaendelea ya kujenga mitambo ya kuzalisha MW 900 pale Kinyerezi ili mara gesi itakapofika umeme uzalishwe.  Hatua hiyo itatuwezesha kuung’oa mzizi wa fitina wa mgao wa umeme na mzigo wa kununua umeme ulio ghali.

Utafutaji wa Gesi
Ndugu Wananchi;
Tangu mwaka 2010 gesi nyingi imegundulika baharini na nchi kavu katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani. Utafutaji bado unaendelea na tuna matumaini kuwa gesi nyingi zaidi huenda ikagundulika.  Hivi sasa Serikali inaandaa sera na sheria mpya ya gesi ili kuboresha zinazotumika wakati huu.  Nia yetu ni kutaka kuhakikisha kuwa rasilimali hii adhimu inasimamiwa vizuri kwa manufaa ya nchi yetu na watu wake pamoja na kulinda maslahi ya wawekezaji.

Napenda kutumia nafasi hii kuwahakikishia ndugu zetu wa kule gesi ilipogunduliwa au popote itakapogundulika, kuwa watanufaika sawia na katu hawatasahaulika.  Rai yao ya kutaka na wao wanufaike inakubalika na Serikali inajiandaa hivyo. Viongozi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara kwa mfano, wanajua maelekezo niliyotoa kuhusu kuiandaa miji ya Mtwara na Lindi kupokea uchumi wa gesi.

Lakini, sharti la kutaka gesi isisafirishwe kwenda kokote na kwamba kila kitu kifanyike kwao halikubaliki. Rasilimali inayopatikana po pote katika nchi hii ni mali ya taifa zima na hutumika kwa manufaa ya taifa.  Katu siyo mali ya watu wa pale ilipogundulika au pale shughuli hizo zinapofanyika. Jumla ya makusanyo ya mapato yatokayo sehemu zote za nchi yetu na kutokana na vyanzo mbalimbali ndiyo yanayotumika kuhudumia watu wote po pote walipo.

Ndugu Wananchi;
 Huu ni msingi mzuri, ni sera nzuri na ni jambo jema la tunu, tulilorithi kwa waasisi wa Taifa letu, ambalo hatuna budi kulienzi na kulidumisha.  Nawasihi wanasiasa wenzangu tusiwaelekeze kwenye mambo mabaya wananchi tunaodai kuwapenda. Kutafuta umaarufu kwa agenda zinazopandikiza chuki kwa watu na kuligawa au kulibomoa taifa, ni upungufu mkubwa wa uongozi na uzalendo.  Tuache siasa za ubarakara na kuwapa watu matumaini yasiyotekelezeka.  Nawaomba wananchi msiwasikilize, si watu wanaowatakia mema na wala hawaitakii mema nchi yetu.

Elimu
Ndugu wananchi;
Tumeendelea kupata mafanikio katika utekelezaji wa sera yetu ya kupanua fursa ya elimu kwa Watanzania katika ngazi zote.  Mwaka huu vijana wetu wengi zaidi walijiunga na elimu ya msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu.  Hivi sasa tunaelekeza juhudi zetu zaidi katika kuongeza ubora wa elimu.    Kwa ajili hiyo, tumechukua hatua za makusudi za kupanua mafunzo na ajira za walimu wa shule za msingi na sekondari.  Kwa mfano,  mwaka huu walimu 24,621 wapya waliajiriwa kati yao 11,379 wa shule za msingi na 13,242 wa shule za sekondari.  Januari, 2013 tunategemea kuajiri walimu 28,746 kati yao 14,606 wa shule za msingi na 14,060 watakuwa wa shule za sekondari.
 Kwa sababu hiyo, uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi umeendelea kuwa mzuri.  Hivi sasa kwa shule za msingi uwiano umefikia 1:46 ukilinganisha na 1:56 mwaka 2005. Uwiano unaostahili ni 1:40. Kwa upande wa sekondari uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi hivi sasa ni 1:29 ukilinganisha na 1:20 unaostahili.  Kutokana na upanuzi wa vyuo vya kufundisha walimu nchini, bila ya shaka baada ya miaka mitatu hivi upungufu wa walimu wa shule za msingi na sekondari haitakuwa kilio tena.

Ndugu Wananchi;
Upatikanaji wa vitabu nao unazidi kuwa bora.  Hivi sasa uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni 1:3 kwa shule ya msingi na sekondari 1:3 ukilinganisha na 1:5 kwa shule za msingi na sekondari 1:4 mwaka 2009.  Hata hivyo, tutaendelea kuongeza mgao wa fedha katika bajeti ya elimu ili kuongeza upatikanaji wa vitabu na vifaa vingine vya kusomea na kufundishia.  Tunataka katika muda mfupi ujao uwiano uwe 1:1.

Kwa upande wa maabara za sayansi, tarehe 4 Novemba, 2012, nilipokuwa kwenye ziara ya Mkoa wa Singida, nilitoa agizo la kutaka ndani ya miaka miwili, kuanzia mwaka 2013, kila shule ya sekondari ya kata nchini iwe na majengo ya maabara yaliyokamilika.  Yawe pia yanatumika kwa maana ya vifaa na mahitaji muhimu.  Nimewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa agizo hili linatekelezwa kwa ukamilifu.  Kuanzia sasa, katika ziara zitakazofanywa Mikoani na mimi, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu tutapenda kupata taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wake.

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa ufundishaji imedhihirika kwamba mkakati maalum unahitajika kuboresha ufundishaji wa masomo ya hisabati, kiingereza na sayansi katika shule za msingi na sekondari.  Matokeo ya mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne kwa miaka mingi sasa yanathibitisha haja hii.  Sasa wakati umefika kwa suala hili kulipa uzito unaostahili.  Tutafanya hivyo kuanzia mwaka 2013.
Afya
Ndugu Wananchi;
Mwaka 2012 ulikuwa na mafanikio mengi ya kutia moyo kwa upande wa sekta ya afya nchini pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali. Kazi ya kusogeza huduma ya afya karibu na wanapoishi watu kwa maana ya kujenga zahanati, vituo vya afya, hospitali mpya na kuimarisha zilizopo iliendelea kutekelezwa kwa mafanikio kote nchini.

Hali kadhalika, uwezo wetu wa ndani wa uchunguzi na tiba ya magonjwa makubwa umezidi kuimarika mwaka huu. Upatikanaji wa dawa, vifaa vya uchunguzi na vifaa tiba umeendelea kuboreshwa.  Aidha, mafunzo na ajira za madaktari, wauguzi na wataalamu wengine wa afya vimeendelea kuongezwa.  Kituo cha Tiba ya Maradhi ya Moyo kimekamilika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mwaka ujao (2013) shughuli za upasuaji na nyinginezo husika kutibu maradhi ya moyo zitakuwa zimeboreshwa sana.  Upanuzi mkubwa wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road umekamilika.  Kwa ajili hiyo, huduma zitakuwa bora zaidi na msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo utakuwa umemalizika.  Ujenzi wa hospitali kubwa ya kisasa katika Chuo Kikuu cha Dodoma unaendelea vizuri na inatarajiwa kukamilika mwaka 2014.  Hospitali hiyo itatumika kufundishia wanafunzi wa udaktari na uuguzi.

Ndugu Wananchi;
  Mwaka huu pia, tumekamilisha matayarisho ya kuanza ujenzi wa hospitali kubwa na ya kisasa kabisa kule Mlonganzila, Dar es Salaam.  Ujenzi utaanza Februari 2013 na kukamilika Februari, 2015.  Hospitali hii pia itakuwa ya kufundishia wakati Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kitakapohamishia sehemu kubwa ya shughuli zake huko Mloganzila.  Mchakato wa ujenzi wa Chuo hicho nao unakaribia kuanza.  Kuwepo kwa hospitali hizi kutaongeza sana uwezo wetu wa ndani wa uchunguzi na tiba.  Sasa naweza kuthubutu kusema kuwa safari ya kupunguza wagonjwa tunawaopeleka nje tumeianza  kwa dhati.

Ndugu Wananchi;
 Tumeendelea kupata mafanikio katika mapambano dhidi ya magonjwa makubwa yanayosababisha vifo vingi kama vile UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria.  Maambukizi na vifo vinazidi kupungua.   Pia vifo vya kina mama na watoto vinaendelea kupungua.

Kwa mujibu wa taarifa za mwaka huu za Shirika la Afya Duniani, vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano hapa Tanzania vimepungua kutoka vifo 81 kwa kila watoto 1000 waliozaliwa hai mwaka 2009 hadi kufika vifo 65.2 mwaka 2011 na vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka vifo 51 kwa kila watoto 1000 waliozaliwa hai mwaka 2009 na kufikia vifo 45 mwaka 2011. Mafanikio haya yanaiweka Tanzania katika orodha ya nchi 10 zinazofanya vizuri duniani katika kupunguza vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Ndugu Wananchi;
   Hatuna budi kufahamu kuwa haya ni matokeo ya kufanya vizuri kwenye chanjo kwa watoto ambayo imefikia wastani wa asilimia 90.  Pia imechangiwa na mafanikio yetu katika kupunguza maambukizi ya malaria na UKIMWI kwa watoto.  Naamini tutapata mafanikio makubwa zaidi kuanzia mwaka 2013 tutakapoanza chanjo dhidi ya kichomi (pneumonia) na ugonjwa wa kuharisha kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.  Aidha, tukiendelea kutekeleza kwa dhati mpango wa kila mtoto kulala kwenye chandarua kilichotiwa dawa na ule Mpango Kabambe wa Kuzuia Maambukizi ya Mama Kwenda kwa Mtoto niliouzindua kule Lindi tarehe 1 Desemba, 2012, mambo yatakuwa vizuri zaidi.
  
Sensa ya Watu na Makazi
Ndugu wananchi;
Leo asubuhi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja nilitangaza matokea ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwezi Agosti, mwaka 2012.  Matokeo haya yanaonyesha kwamba idadi ya watu nchini Tanzania ni milioni 44,929,002 kati yao watu milioni 43,625,434 wanaishi Tanzania Bara na milioni 1,303,568 wanaishi Zanzibar.  Ukilinganisha na Sensa ya mwaka 2002 tulipokuwa na watu milioni 34.4, hili ni ongezeko la watu milioni 10.5 au wastani wa asilimia 2.6 kwa mwaka.
Matokeo haya yana maana kubwa kwa Serikali na kwa kila mmoja wetu.  Kwa kasi hii ya ongezeko la watu ifikapo mwaka 2016 Tanzania itakuwa na watu milioni 51.6.  Hii ni idadi kubwa sana ya watu inayoleta changamoto kwa Serikali na jamii.  Hatuna budi kutambua maana ya idadi hiyo ya watu na kujipanga vyema kukidhi mahitaji yao na hasa kuhakikisha kuwa maskini hawaongezeki na huduma zinatosheleza mahitaji na zina ubora wa juu.  Kazi hiyo lazima ianze sasa na ionekane katika Mipango ya Maendeleo.

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wetu, sisi wananchi, taarifa hii inamlazimu kila mmoja wetu atambue kuwa kwa kasi hii, siku za usoni nchi yetu itakuwa na watu wengi, hivyo ushindani kwa rasilimali utakuwa mkubwa.  Watakaofanikiwa wakati huo ni wale wenye familia ndogo au zile ambazo zimepanga uzazi.  Tukipanga uzazi tunajipa nafasi ya kutunza na kulea vizuri watoto wetu na kuwapatia mahitaji yao muhimu ya maisha.

Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii kurudia kuwashukuru wananchi wenzangu wote kwa ushirikiano wenu uliowezesha zoezi zima kufanikiwa kiasi hiki.  Aidha, nawashukuru kwa dhati viongozi, watendaji wakuu na maofisa wote waliopanga, kuratibu, kusimamia na kutekeleza zoezi la kuhesabu watu.  Natoa shukrani maalum kwa Kamati ya Kitaifa ya Sensa, Kamati za Sensa za Mikoa na Wilaya, Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Jamhuri ya Muungano na Afisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar na makarani wote wa sensa.  Penye nia pana njia.  Tumeweza kushinda changamoto zote na kuwapatia Watanzania nyenzo muhimu ya kupanga mipango ya maendeleo yao.

Vitambulisho vya Taifa
Ndugu wananchi;
Mwaka huu tumeanza zoezi la kusajili watu na makazi kwa ajili ya kuandaa kutoa Vitambulisho vya Taifa kuanzia mwaka 2013.   Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ilifanya zoezi la majaribio katika mkoa wa Dar es Salaam na wilaya ya Kilombero ambalo lilifanikiwa.  Hivi sasa wanaendelea na zoezi hilo Zanzibar. Maandalizi kwa ajili ya kutekeleza zoezi la kutoa vitambulisho nchi nzima kuanzia mwaka 2013 yanakwenda vizuri.   Napenda kuwasihi wananchi wenzangu wakati utakapofika kutoa ushirikiano unaostahili kwa maafisa watakaohusika na kukusanya taarifa na kutoa vitambulisho ili zoezi lifanikiwe ipasavyo.  Nawaomba muitumie vizuri fursa hii ya kujisajili na kupata vitambulisho.

Mchakato wa Katiba Mpya
Ndugu wananchi;
Mtakumbuka kuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nililiyoiunda tarehe 1 Mei, 2012 ilianza kazi yake rasmi tarehe 29 Juni, 2012 na inaendelea vyema.  Mpaka sasa Tume imekamilisha hatua ya kwanza ya kukusanya maoni ya mtu mmoja mmoja katika Mikoa yote nchini.  Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni.  Zoezi linalofuata ni la kukusanya maoni ya makundi maalumu kuanzia mwezi  Januari, 2013.  Natoa wito kwa makundi hayo nayo kushiriki vizuri kwenye hatua hii muhimu.  Baada ya hatua hiyo kukamilika, Tume itaandaa Rasimu ya Katiba ambayo wanategemea itakuwa tayari mwezi Mei, 2013.

Ndugu Wananchi;
Kwa mujibu wa ratiba ya Tume, rasimu hiyo itawasilishwa kwenye Vikao vya Mabaraza ya Katiba vitakavyofanyika kati ya mwezi Juni na Agosti, 2013.    Tume itatangaza muundo na namna ya kuwapata Wajumbe wa Mabaraza hayo na utaratibu utakaotumika wakati wa kujadili na kutoa maoni juu ya Rasimu ya Katiba wakati huo ukiwadia.

Baada ya kukamilika kwa Vikao vya Mabaraza ya Katiba, Tume itakamilisha Rasimu ya Katiba ambayo itachapishwa kwenye Gazeti la Serikali kama yalivyo matakwa ya Sheria.  Aidha, itachapishwa katika magazeti ya kawaida kwa wananchi kusoma.  Mwezi Novemba, 2013 rasimu hiyo itawasilishwa kwenye Bunge Maalum kujadiliwa na kupitishwa.  Baada ya Bunge Maalum kupitisha Rasimu ya Katiba, Rasimu hiyo itapelekwa kwa wananchi kwa uamuzi wa mwisho kupitia kura ya maoni.

Ndugu Wananchi;
   Matarajio yetu ni kwamba kama kila kitu kitakwenda kama inavyotarajiwa nchi yetu itakuwa na Katiba Mpya iliyotokana na maoni na matakwa ya wananchi ifikapo mwaka 2014.  Mwaka huo Muungano wetu utakuwa unatimiza miaka 50 hivyo hiyo itakuwa zawadi ya tunu kubwa.  Tukifanikiwa kupata Katiba mpya wakati huo, tutafanya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa kutumia Katiba hiyo.  Inshallah, Mwenyezi Mungu atajaalia baraka zake, nia yetu njema itatimia.  Pamoja na hayo, natoa wito kwenu wananchi wenzangu kushiriki kwa ukamilifu katika hatua zote za mchakato ili tuweze kujenga muafaka kuhusu Katiba tunayoitaka.

Marekebisho ya Sheria
Ndugu Wananchi;
Katika hotuba yangu ya mwisho wa mwezi wa Februari, 2012, nilieleza kwamba katika mazungumzo baina ya Serikali na  vyama vya siasa na wadau wengine juu ya marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tulikubaliana tushughulikie marekebisho ya Sheria hiyo hatua kwa hatua.   Tulikubaliana kuanza na mambo yanayohusu Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Wananchi ili Tume iundwe na ianze kazi.  Baada ya hapo tuangalie vipengele vinavyohusu Bunge Maalum na Kura ya Maoni.  

Tulifanya hivyo kuhusu Tume ya Katiba na sasa tunajiandaa kuanza mazungumzo kuhusu ngwe iliyobaki yaani, Bunge Maalum na Kura ya Maoni.  Kama mazungumzo yatakamilika mapema kunako Januari, 2013 mapendekezo hayo yatafikishwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano katika kikao cha Februari   kwa uamuzi.  Vinginevyo itakuwa katika Bunge la Aprili, 2013

Ndugu Wananchi;
Kuhusu Kura ya Maoni, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inaelekeza kuwa Kura ya Maoni itatungiwa Sheria yake maalum.  Ni matumaini yangu kuwa matayarisho yake yataanza mapema iwezekanavyo.  Nawasihi wananchi wenzangu, viongozi wa vyama vya siasa na asasi za kijamii tuwe watulivu, tuendelee kushirikiana katika mchakato huu wa Katiba mpaka tulifikishe jahazi ufukweni salama kwa mustakabali mwema wa nchi yetu na watu wake.

Mfumo wa Dijitali
Ndugu wananchi;
Bila ya shaka mtakumbuka taarifa za Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Tume ya Mawasiliano kwamba kuanzia tarehe 1 Januari, 2013 nchi yetu itahamia katika mfumo wa mawasiliano unaotumia teknolojia ya dijitali (au kidijiti kwa tafsiri ya BAKITA) badala ya huu wa sasa wa analojia. Uamuzi huu unakuja kufuatia uamuzi wa kimataifa kwamba nchi zote duniani ziwe zimeingia kwenye mfumo huu ifikapo mwaka 2015.  Pia unazingatia uamuzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa nchi zetu kuanza safari hiyo tarehe 1 Januari, 2013.

  Hapa nchini zoezi hili litafanyika kwa awamu.  Litaanza katika mikoa saba ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mbeya, Kilimanjaro, Mwanza na Tanga na mingine itafuata kwa mujibu wa ratiba itakayopangwa.

Ndugu Wananchi;
 Teknolojia ya dijitali katika mfumo wa mawasiliano hufanya picha za televisheni kuwa nzuri na hazina chenga chenga.  Mawasiliano ya simu yatakuwa mazuri zaidi.  Vile vile, itakuwa rahisi kupata huduma za televisheni kwenye simu za mkononi na huduma ya intaneti kwenye televisheni.

Ndugu Wananchi;
Ili kuweza kutumia teknolojia hii, kila televisheni inatakiwa iwe na kifaa kiitwacho king’amuzi. Vifaa hivi vipo kwa wingi madukani na wengine tayari wanavyo. Naomba niwatoe hofu kwamba kwa kuingia katika mfumo huu siyo lazima kununua televisheni mpya. Televisheni yo yote yenye vitundu vitatu vya rangi za njano, nyeupe na nyekundu itaweza kufanya kazi kwenye mfumo wa dijitali. Hata wale ambao hawana televisheni za namna hiyo wanaweza kununua kifaa cha kuunganishia king’amuzi na mambo yakawa mazuri.

Uhusiano wa Kimataifa
Ndugu wananchi;
Katika mwaka 2012, uhusiano wetu na washirika wetu wa maendeleo ulikuwa mzuri na uliendelea kuimarika.  Wote wanaridhika na kusifu kazi nzuri inayofanywa na Serikali yetu na ndiyo maana wanaendelea kushirikiana nasi na kutoa misaada ya maendeleo.  Aidha, wameonesha nia thabiti ya kuendelea kushirikiana nasi na kutusaidia katika harakati zetu za kujiletea maendeleo.

Napenda kutumia nafasi hii kwa niaba yenu nyote kutoa shukrani za dhati kwa washirika wetu wa maendeleo kwa mchango mkubwa wanaoendelea kutoa kwa maendeleo ya nchi yetu.  Nawahakikishia kuwa tunathamini sana ushirikiano wao na misaada yao na tutafanya kila tuwezalo kudumisha ushirikiano baina yetu.

Mkutano wa Smart Parntership
Ndugu Wananchi;
Mwaka huu nchi yetu ilipata bahati ya kuwa mwenyeji wa mikutano mikubwa ya kikanda na kimataifa.  Mikutano hiyo ni pamoja na Mkutano Mkuu wa Shirika la Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA), Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Mkutano Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Chanjo (GAVI) na Mkutano wa Wakuu wa Nchi za  SADC.

Bahati nzuri mwaka 2013 Tanzania itakuwa mwenyeji wa mikutano mingine ukiwemo ule wa Global 2013 Smart Partnership Dialogue utakaofanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 24 – 28 Mei, 2013.  Huu ni mkutano unaohusisha nchi nyingi duniani na kutoka takriban mabara yote.  Mkutano huu hukutanisha na kushirikisha viongozi wa Serikali wakiwemo Wakuu wa Nchi na Serikali, viongozi wa sekta binafsi wakiwemo wa makampuni makubwa ya kimataifa, wasomi  na wawakilishi wa asasi za kiraia na watu binafsi.

Kwa kawaida katika mkutano kama huu huwepo agenda maalum, aghalabu kuhusu masuala ya uchumi, biashara na maendeleo.   Mkutano wa mwaka 2013 utazungumzia “Matumizi ya Sayansi na Teknolojia kwa Ajili ya Maendeleo ya Afrika” (Leveraging Science and Technology for Africa’s Development).  Kwa kweli ni kipaumbele muafaka kabisa, ndiyo maana na sisi tumefarijika kuukaribisha.

Ndugu Wananchi;
Kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa kama huu wa watu zaidi ya 500 mashuhuri, ni heshima kubwa kwa nchi yetu.  Ni nafasi nzuri ya kuitangaza Tanzania na fursa zake za uwekezaji, biashara na utalii. Pia, ni nafasi nzuri kwa wafanyabiashara wetu kutangaza shughuli zao na fursa za biashara na uwekezaji wanazotaka kushirikisha wafanyabiashara wa nje.  Naomba tuitumie vyema fursa hiyo adimu kwa manufaa ya taifa na ya waanyabiashara wetu.   Tuwaonyeshe wageni wetu upendo na ukarimu kama ilivyo sifa yetu Watanzania ili waondoke na kumbukumbu nzuri za nchi yetu na watamani kurudi tena kutembea au kuwekeza.
 
Hitimisho
Ndugu wananchi;
Tunatarajia kuwa mwaka 2013 utakuwa mwaka wa mafanikio makubwa zaidi katika nyanja zote kuzidi mwaka 2012.  Mambo yaliyokwama mwaka 2012 yatakwamuliwa.   Ajira zitaongezeka kwa uwekezaji vitega uchumi kuongezeka na kuwajengea uwezo wajasiriamali wazalendo, ili waweze kujiajiri wenyewe na kuajiri wengine.  Kwa ajili hiyo, Mifuko ya kusaidia wajasiriamali wadogo, wanawake na vijana itafufuliwa na kutengewa fedha nyingi katika bajeti ya Serikali.
 Mwaka 2013 ni mwaka wa matumaini, hivyo kila mmoja wetu anatakiwa kujituma na kutimiza wajibu wake.  Maisha bora yatakuja kwa kila mmoja wetu kutimiza wajibu wake ipasavyo.  Kama kila mtu atafanya kazi kwa bidii na maarifa, na, kama kila mmoja wetu atajivunia matokeo ya kazi yake na siyo uhodari wa maneno yake ya uchambuzi wa hali.  Kila mtu achukie uvivu na tabia ya kulalamika pasipo kufanya kazi.

Ndugu Wananchi;
Mimi na wenzangu Serikalini tunawaahidi ushirikiano wa hali ya juu na kwamba tutawatumikia kwa moyo wetu wote, kwa nguvu zetu zote na kwa maarifa yetu yote.  Tunataka kukidhi matarajio na imani ya wananchi kwa Serikali yao. Tutaendelea kuimarisha utendaji kazi Serikalini na kuhimiza uwajibikaji katika ngazi zote za uongozi. Tutaendeleza mapambano dhidi ya rushwa bila ajizi na watumishi wasio waaminifu, wazembe, wabadhirifu wa mali ya umma watawajibishwa ipasavyo.  Wananchi pia wanao wajibu wa kuwa raia wema na wazalendo wa kweli kwa nchi yao. Kila mmoja wetu ajiulize ataifanyia nini jamii yake na nchi yake badala ya kuuliza itamfanyia nini.

Ndugu zangu,Watanzania Wenzangu;
Nawatakieni nyote heri na fanaka tele katika mwaka mpya wa 2013. Tusherehekee pamoja kwa amani na utulivu.

Mungu Ibariki Afrika!
   Mungu Ibariki Tanzania!
        Asanteni sana kwa kunisikiliza.