HABARI

 

Thursday, September 19, 2013

BAADHI YA MAGAZETI LEO IJUMAA SEPT. 20, 2013

1 Comments












©2013 theNkoromo Blog

Read more...

DK. MNDOLWA: MIKAKATI KAMABE INASUKWA KUBORESHA SHULE ZILIZOPO CHINI YA JUMUIA YA WAZAZI YA CCM

0 Comments
NA MWANDISHI WETU, TANGA
MWENYEKITI wa Jumuia ya wazazi mkoani Tanga, Dk. Edmund Mndolwa, amesema kuna mikakati ya haraka ya kuboresha shule za jumuia hiyo ili ziweze kutoa elimu bora.

Alisema shule za jumuia ya wazazi zilikuwa kimbilio la wazazi na Watanzania kwa jumla, lakini kwa sasa zinakabiliwa na soko la ushindani kutokana na shule nyingi za kata na binafsi.

Akizungumza katika ziara ya kutoa shukrani katika mkoa wa Tanga kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dk. Mndolwa alisema shule za wazazi zote nchini zinakabiliwa na uhaba wa walimu, vitendea kazi na vitabu.

Alieleza kuwa shule hizo zimekuwa na tatizo la mfumo wa uendeshaji wake, kitu kinachochangia kujiendesha kiholela na wakuu wa shule kuzichukulia kama zao.

“Tunatakiwa kubadilika na kuzirejesha shule zetu katika hali yake ya zamani. Kwa kufanya hivyo, tutawafanya Watanzania waendelee kuzikimbilia shule hizo ambazo zilikuwa mkombozi kwao,

“Tushirikiane kuanzia wazazi kwa kulipa ada ili walimu wapate mishahara mizuri na wakipata mishahara mizuri watafundisha kwa ari na moyo, hivyo hata watoto wetu watapata elimu nzuri,”alieleza Dk. Mndolwa.

Dk. Mndolwa alisema kuwa mkoa wa Tanga una shule za wazazi sita huku nchi nzima kukiwa na shule za wazazi 71.

Aidha, akizungumza katika wilaya za Mkinga, Muheza  na Pangani, Dk. Mndolwa aliwataka viongozi wa jumuia hiyo kuwa watumishi wa watu kwa kwenda kusikiliza kero zao katika ngazi za chini badala ya kujifungia ofsini.

Vilevile, aliwataka viongozi hao kuachana na dhuluma kwa wanachama wanapokuwa wanaomba nafasi ya uongozi, kwani kwa kuendeleza dhuluma kunachangia kupunguza nguvu ya chama.

“Unakuta mwanachama anakubalika na wananchi lakini kwa sababu ya chuki na dhuluma anapewa mtu mwingine ambaye hakuongoza kura za maoni, hali ambayo hujenga chuki kwa wanachama na kuamua kuwapigia kura wapinzania,

“Ukiangalia, nafasi nyingi tulizopoteza katika ngazi mbalimbali kuanzia wenyeviti wa serikali za mitaa, udiwani na ubunge, nafasi nyingi zimetokana na dhuluma, na waliowachagua wapinzania ni wanaCCM wenyewe kwa sababu ya kuchukizwa kwa mtu waliyempenda kutorudishwa jina lake,”alieleza.
Read more...

ZIARA YA KINANA SIMIYU, AONYESHA MFANO WA VIONGOZI KUJICHANGANYA NA WANANCHI

0 Comments

  • ASEMA CCM HAITAKUBALI KUBURUZWA
  • ASEMA CHADEMA NI MANENO TU, HAICHANGII CHOPCHOTE KATIKA MAENDELEO
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubeba matofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya balozi Joyce Safari  wa shina namba 12 tawi la Isenge kata ya Dutwa.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakichimba msingi wa ujenzi wa nyumba ya balozi Joyce Safari wa shina namba 12 Tawi la Isenge kata ya Dutwa.
 Balozi Joyce Safari wa shina namba 12 tawi la Isenge kata ya Dutwa akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye shina lake.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa amekaa pamoja na wakazi wa tawi la Isenge kata ya Dutwa wilaya ya Bariadi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakazi wa tawi la Isenge baada ya kutembelea shina namba 12 kata ya Dutwa wilaya ya Bariadi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa tawi la Isenge kata ya Dutwa juu ya umuhimu wa ushirikiano na mshikamano kwa wananchi na wanachama wa CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk.Titus Kamani,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti na Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge wakila chakula cha Asili aina ya Michembe pamoja na Balozi Joyce Safari wa Shina namba 12 kata ya Dutwa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimimina maharage kwenye wali uliokuwa kwenye tayari kula na wananchi pamoja na viongozi wengine.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akila pamoja na wananchi wa tawi la Isenge kata ya Dutwa baada ya kushiriki nao ubebaji wa matofali na uchimbaji wa msingi wa nyumba ya Balozi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akipokea taarifa ya soko la mazao ya kilimo na mifugo la Igaganulwa kata ya Dutwa .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia na mmoja wa wafanya biashara katika soko la Igaganulwa kata ya Dutwa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia samaki aina ya furu katika soko la Igaganulwa alipokuwa ziarani wilaya ya Bariadi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi na wafanya biashara katika soko la Igaganulwa kata ya Dutwa wilaya ya Bariadi ambapo aliwaeleza wananchi hao umuhimu wa kushirikiana na viongozi wao katika kutatua matatizo yao na kupanga kuleta maendeleo na kujiepusha na wanasiasa ambao mtaji wao ni maneno na si mipango ya maendeleo.

 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman KInana akishiriki katika ujenzi wa Madarasa ya shule ya sekondari ya MAlambo wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.
 Kikundi cha Ngoma cha Maisha Furaha Group kikitumbuiza kwa ngoma ya Bugobogo katika viwanja vya sabasaba wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM alihutubia.

 Mbunge wa Bariadi Ndugu Andrew Chenge akihutubia wakazi wa Bariadi wakati wa mkutano wa Hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya sabasaba wilayani hapo.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk.Titus Kamani pamoja na Mbunge wa Bariadi Ndugu Andrew Chenge wakiwasalimu wakazi Bariadi waliofurika kwenye viwanja vya sabasaba wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Bariadi na kuwaambia CCM imejipanga kutekeleza ahadi zake zaidi kuliko malumbano.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Bariadi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba .
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu kuwasha pikipiki moja kati ya pikipiki tano ambazo walikabidhiwa vijana wa Bodaboda mjini hapo. PICHA NA ADAM MZEE
Read more...

Tuesday, September 17, 2013

KINANA, NAPE WAPATA HESHIMA YA UKAZI WILAYA MPYA YA ITIMILA, MKOA MPYA WA SIMIYU

0 Comments
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na viongozi wengine akiwa amekaa baada ya kusimikwa tena kuwa Chifu wa Wasukuma eneo la Migato, Itimila, leo. 
Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahaman Kinana akinywa kahawa aliyoinunua baada ya kuwasili  katika Kijiji cha Budalabujiga,wilaya mpya ya Itimila,mkoani Simiyu leo katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani chama.
Katibu wa  Itikadi  na Uebnezi wa CCM, Nape Nnauye akinywa kahawa katika Kijiji hicho
Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahaman Kinana akihutubia  wananchi baada ya kuwasili  katika Kijiji cha Budalabujiga,wilaya mpya ya Itimila,mkoani Simiyu leo katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani chama.
Kinana akikagua moja ya vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Kanadi katika Kijiji cha Nanga wilauyani Itimila
 Kinana akiwahimiza wanafunzi wa Shule ya Kanadi kusoma sana masomo ya sayansi
Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Simiyu,Njalu Silanga akitangaza kuchangia fedha kwa ajili ya kuweka kuweka umeme wa jua pamoja na kununua TV kwa ajuli ya shule ya Kanadi wilayani Itmila leo
 Nape akiwa na mtoto waliyemkuta na mamake katika Zahanati ya Nangale  Katika Kata ya Ndolelezi
Kinana akiondoka baada ya kukagua Zahanati ya Nangale, wilayani Itimila
 Kinana akikangalia maginia ya mahindi yaliyohifadhiwa katika ghala la Kikundi cha  Saccos katika Kijiji cha Mwanihunda wilayani humo. Kila mwananchi anayehifhadhi katika ghala hilo hulipa kila gunia sh. 100 kwa mwezi.
Kinana akisimikwa tena kuwa Mtemi wa Migato alipozungumza na wanachama wa shina namba 15 la Migato wakati wa ziara yake wilwywni Itimila leo. Alichangisha sh. mil. 3.6 za kutunisha mfuko wa Saccos ya Shina hilo.
Kinana akiwa amekaa huku akiwa amaevalia kitemi na fimbo yake.
Akinywa maji kwa kutumia kikombe cha jadi
Kinana  na viongozi wengin wakila chakula cha asili cha kabila la wasukuma cha Mchembe kinachotokana na viazi vilivuokaushwa
Kinana akisaidia kupiga plasta jengo la Ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya mpya ya Itimila
Kinana akiapandamtu katika kiwanja patakapojengwa ofisi za Mkuu wa Wilaya mpya ya Itimila
Makao Makuu ya Muda ya Ofisi  Mkuu wa Wilaya ya Itimila
Dereva wa msafara wa Kinana akisaka mtandao kabla ya kuanza kupiga simu. Katika wilaya hiyo mpya inapatikana mitandao ya Vodacom  na Tigo
Kinana akiwa katika mkutano wa wandani na wanachama wa wilaya hiyo
 Kwaya ikitumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara katika makao Makuu ya wilaya hiyo
Katibu wa Utikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo wa hadhara


Read more...