HABARI

 

Monday, August 19, 2013

BARAZA LA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA LAKUTANA

0 Comments
Baadhi ya wawezeshaji wakijadiliana jambo katika Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba Baadhi ya washiriki wa Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba Mmoja wa washiriki wa warsha katika Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba akijadili jambo Warsha ya wajumbw wa Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba ikiendelea [/caption] BARAZA la Mtandao wa Wanawake limekutana lililoshirikisha wajumbe kutoka mikoa mbalimbali limekutana kwa siku mbili kujadili masuala ikiwemo namna ya ushiriki wa wanawake katika mabaraza yanayojadili rasimu ya Katiba Mpya. Kwa mujibu wa vyanzo wa habari hizi washiriki hao walikutana kwa siku mbili, yaani Agosti 16 na 17 mwaka huu Makao Makuu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa mada zilizowasilishwa na kujadiliwa na wajumbe wa warsha hiyo ni pamoja na Mchakato wa Katiba Mpya na Ushiriki wa Wanawake katika Hatua mbalimbali, ikiwemo uchambuzi wa rasimu ya Katiba Mpya iliyowasilishwa na Diana Kidala wa Jukwaa la Katiba na mada ya Umuhimu wa Kuwepo kwa Sauti za Wanawake katika Katiba Mpya iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya. Mada zingine zilizowasilishwa na kujadiliwa na wajumbe hao ni pamoja na Uwasilishaji wa Masuala Muhimu ya Kijinsia yaliyojitokeza katika rasimu ya Katiba Mpya ya Mkurugenzi Mtendaji wa WFT, Mary Rusimbi na ile ya Masuala Muhimu ya Wanawake ya Kuiimarishwa na Kuingizwa katika Katiba Mpya iliyowasilishwa na Vicky Lihiru kutoka ULINGO. Pamoja na mambo mengine pia wajumbe hao walijenga mikakati ya pamoja kuendeleza ushiriki wa mtandao katika hatua zinazofuata kwenye mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya yenye mrengo wa usawa wa jinsia nchini. Baraza hilo la wajumbe lilifungwa na Bi. Betty Minde kutoka KWIECO. *Imeandaliwa na www.thehabari.com
Read more...

Sunday, August 18, 2013

MBOWE AWAHIMIZA WATANZANIA KUTOA MAONI RASIMU YA KATIBA MPYA

0 Comments
IMG_2543
Helikopta maalum iliyowabeba viongozi wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh. Freeman Mbowe pamoja na Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika walipowasili eneo la Mnada Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kufanya mkutano wa hadhara wilayani humo mwishoni mwa Juma. (Picha na Zainul Mzige wa Dewji Blog).
IMG_2579
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh. Freeman Mbowe akihutubia wakazi wa wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza mwishoni mwa juma kwenye mkutano wa hadhara. (Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).
IMG_2610
Mwananchi wa Geita ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akitoa maoni yake ya Rasimu ya Katiba Mpya mbele umati wa wafuasi wa Chadema na wakazi wa wilaya hiyo ambapo wengi wao wametaka Ushuru wa Masoko ufutwe pamoja na baadhi ya kinamama kulalamikia shida ya Maji kwenye Wilaya hiyo na Mh.Mbowe aliwaasa kutumia Mabaraza ya CHADEMA kuwasilisha maoni yao wakati wa mkutano wa hadhara.
IMG_2604
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika akiteta jambo na mmoja wa viongozi wa Chadema wilayani Sengerema Hemedi Sabula wakati wa mkutano huo wa hadhara.
Read more...

Monday, August 12, 2013

KINANA AKUTANA NA BALOZI WA CANADA NA MKURUGENZI WA TAASISI YA NDI YA MAREKANI

0 Comments

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti 12, 2013. Balozi huyo alipomtembelea na kuwa na mazungumzo naye. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro..
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimwelewesha jambo Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque, alipomkaribisha Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti 12, 2013. Balozi huyo alipomtembelea na kuwa na mazungumzo naye. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque, alipomkaribisha Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti 12, 2013.  Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsindikizaa Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque, baada ya mazungumzo  yao, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti 12, 2013
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque, baada ya mazungumzo yao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti 12, 2013.

MKUREUGENBZI WA NDI KUSINI NA MASHARIKI MWA AFRIKA
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mkurugenzi wa Taasisi ya Chama Cha Democrat cha Marekani, inayojishughulisha na programu mbalimbali za mamboresho ya kisiasa (NDI), Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dk. Keith Jennings, mgeni huyo alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo na kuwa na mazungumzo. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose Migiro.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi ya Chama Cha Democrat cha Marekani, inayojishughulisha na programu mbalimbali za mamboresho ya kisiasa (NDI), Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dk. Keith Jennings, mgeni huyo alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Agosti 12, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose Migiro.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Chama Cha Democrat cha Marekani, inayojishughulisha na programu mbalimbali za mamboresho ya kisiasa (NDI), Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dk. Keith Jennings (watatu kushoto), baada ya mazungumzo na  mgeni huyo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Agosti 12, 2013. (Wapili Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose Migiro.Wengine ni ujumbe aliofuatana nao Mkurugenzi huyo. Ofisa Mkuu wa Programu wa NDI Kusini na Mashariki mwa Afrika, Martha Haile (kushoto) na kulia ni Ofisa wa Programu wa NDI, Tanzania, Mahija Dodd na Dk. Bernadeta Killian kutoka Idara ya Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Imetayarishwa na theNkoromo Blog
Read more...

Thursday, August 8, 2013

WAPINZANIA WACHEZEA KICHAPO KIBONDO

0 Comments
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akizungumza na madiwani wa CCM wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wiki iliyopita.

WAPINZANI WACHEZEA KICHAPO KIBONDO
Katika hali inayothibitisha ule usemi wa mwanamuziki Chamilion wa Uganda kuwa "fitina yako bahati yangu" wapinzani wamechezea kichapo cha mwaka kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kibondo baada ya CCM kushinda kwenye nafasi zote za kuongoza Halmashauri hiyo, ushindi uliowaacha midomi wazi wapinzani waliokuwa wakisubiri kufaidi kwenye ugomvi wa madiwani wa CCM wilayani hapo.

Diwani wa CCM Ndugu  Emily Msanya kuibuka Mwenyekiti wa Halmashauri baada ya kupata kura 14 kati ya 17 zilizopigwa na Makamu Mwenyekiti ni Apronary Mazinda ambaye pia alishinda kwa kura 14 kati ya 17.

Kuchaguliwa kwa madiwani hao na ushindi huo wa CCM kwenye ngome ya upinzani ambapo Mbunge wa jimbo hilo ni Ndg. Mkosamali wa NCCR-Mageuzi ni uthibitisho dhahiri kuwa CCM ina mkakati mkubwa wa kuzidhibiti ngome zote za upinzani nchini kuelekea uchaguzi wa 2014 na 2015.

Kabla ya uchaguzi huo palikuwa na mgogoro mkubwa kati ya madiwani wa CCM, mgogoro ambao ulitatuliwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye kufuatia ziara yake ya kimyakimya ya siku moja wilayani Kibondo ambapo alikutana na madiwani hao wa CCM kwa zaidi ya masaa manne.

Matokeo haya ni kinyume kabisa na kile kilichoandikwa na Gazeti la Tanzania Daima la Agosti 7,2013 kuwa ' WIKI NGUMU KWA CCM" wakieleza kuwa CCM wangepoteza uchaguzi huu. Fitina hiyo ya TanzaniaDaima imegeuka kuwa bahati kwa CCM maana imetembeza kichapo cha haja kwenye uchaguzi huo.

Nape akiongea juu ya ushindi huo akinukuliwa na redio moja ya Mjini Mwanza alisema "ushindi huo ni mawingu mvua zenyewe zinakuja. Unajua hawa jamaa wanawekeza kwenye migogoro ndani ya CCM ili ikitokea hatukuelewana mahali basi wanazamia, hapa nimewazidi akili" alikaririwa Nape.
Read more...